Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Abdi Hija Mkasha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Micheweni

Primary Question

MHE. ABDI HIJA MKASHA aliuliza:- Je, Kamera zilizofungwa Mji Mkongwe Zanzibar zinasaidiaje katika kupambana na kudhibiti uhalifu kwenye maeneo haya?

Supplementary Question 1

MHE. ABDI HIJA MKASHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini nina swali dogo moja la nyongeza. Je, ni lini Serikali itafunga kamera za usalama katika Miji ya Pemba ikiwemo na Wilaya ya Micheweni? (Makofi)

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Abdi Hija Mkasha, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa kwa upande wa Pemba, tayari kamera zimeshafungwa kwenye Mji wa Chakechake, Mkoani pamoja na Wete. Vilevile, katika Mwaka wa Fedha 2025/2026, tumetenga fedha kwa ajili ya kumalizia maeneo yaliyobaki ikiwepo Mji wa Micheweni.