Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 6 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 74 2025-04-15

Name

Ally Mohamed Kassinge

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilwa Kusini

Primary Question

MHE. ALLY M. KASSINGE aliuliza:-

Je, nini mpango wa kujenga kwa kiwango cha lami Barabara ya Kiranjeranje – Nanjirinji hadi Ruangwa kwa kuanza kipande cha Kiranjeranje – Makangaga?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeanza ujenzi wa Barabara ya Kiranjeranje – Makangaga – Nanjirinji hadi Ruangwa yenye urefu wa kilometa 120 kwa kuanza na ujenzi wa madaraja makubwa matatu (3) kwa kutumia fedha za dharura zilizotoka kwenye mkopo nafuu wa Benki ya Dunia. Madaraja haya ni Kigombo lenye urefu wa mita 25, utekelezaji wake umefikia 25%, Daraja la Nakiu lenye urefu wa mita 70, kandarasi yake ipo kwenye maandalizi ya ujenzi na Daraja la Mbwemkuru III lenye urefu wa mita 100 lipo katika hatua ya mapitio ya usanifu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati ujenzi wa madaraja haya matatu unaendelea, Serikali inaendelea kutafuta fedha ili kujenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami. Ahsante.