Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Ally Mohamed Kassinge

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilwa Kusini

Primary Question

MHE. ALLY M. KASSINGE aliuliza:- Je, nini mpango wa kujenga kwa kiwango cha lami Barabara ya Kiranjeranje – Nanjirinji hadi Ruangwa kwa kuanza kipande cha Kiranjeranje – Makangaga?

Supplementary Question 1

MHE. ALLY M. KASSINGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa majibu ya Serikali. Hata hivyo, nina maswali madogo mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; kwa kuwa ujenzi wa madaraja haya matatu ambayo Mheshimiwa Waziri amezungumza, kasi yake ni ndogo; je, Serikali haioni umuhimu wa kuharakisha ujenzi wa madaraja haya ili barabara hii iweze kupitika kipindi chote cha mwaka?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; kipande cha kutoka Kiranjeranje mpaka Makangaga ni kipande ambacho kimejengwa kwa mawe, kitu ambacho kinaathiri sana magari yetu ambayo yanakwenda kuchukua madini ya gypsum kule Makangaga. Je, kwa nini Serikali isione umuhimu wa kujenga kipande hiki angalau kwa kiwango cha changarawe wakati tunatafuta fedha kwa ajili ya kujenga kwa kiwango cha lami? (Makofi)

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba ujenzi wa haya madaraja yote matatu kwa sasa, kwanza tunakamilisha usanifu. Pia, madaraja haya mengine ni kati ya madaraja ambayo tunajua mito mingi sasa hivi inapeleka maji baharini na ni kati ya madaraja ambayo maji hayo yanapita.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna uhakika kwamba, mvua itakapokuwa imepungua na kwa sababu tuna uhakika sana na wakandarasi na chanzo cha fedha, mara tu mvua zitakapokatika, tutahakikisha kwamba madaraja haya yanakamilika. Nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge, madaraja haya mkataba ni yakamilike ndani ya mwaka mmoja. Kwa hiyo, tutahakikisha kwamba, tunasimamia ili madaraja haya yaweze kukamilika kwa wakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu ujenzi wa hiki kipande alichokitaja, tunatambua kwamba ni kweli huku ndiko kunakotoka gypsum kwa sehemu kubwa na magari yanayopita kule ni magari mazito sana. Wizara imeendelea kulifanyia mchakato ili tuone kujenga barabara ambayo itakuwa na uwezo wa kubeba hayo magari mazito ambako kunatoka hiyo gypsum.

Name

Ritta Enespher Kabati

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ALLY M. KASSINGE aliuliza:- Je, nini mpango wa kujenga kwa kiwango cha lami Barabara ya Kiranjeranje – Nanjirinji hadi Ruangwa kwa kuanza kipande cha Kiranjeranje – Makangaga?

Supplementary Question 2

MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Barabara ya Kitonga ni muhimu sana kwa Uchumi wa Nchi hii kwa sababu inaunganisha Tanzania na lango la SADC. Hata hivyo, hii barabara ujenzi wake unasuasua kiasi kwamba magari yana-park pale mpaka saa tatu hadi nne. Je, nini mkakakti wa Serikali ili kuhakikisha kwamba barabara hii haina mkwamo na inapitisha magari kila wakati? Ahsante sana.

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba, tutambue kuwa hii barabara ndiyo kati ya Barabara Kuu (T1) ya kutoka Dar es Salaam kwenda Tunduma na ni kati ya barabara ambazo zinashikilia uchumi wa nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, tuna option mbili. Moja, ni kuipanua hiyo barabara (hicho kipande) kuwa walau njia tatu. Ni eneo ambalo lina milima na miamba na tunaendelea na mkandarasi na tunategema pengine tuongeze mkandarasi mwingine ili tuweze kuongeza kasi ya kutengeneza. Vilevile, suala lingine tunaangalia uwezekano kama tunaweza tukajenga barabara nyingine ya mchepuko ili incase panafunga, basi tuwe na namna nyingine ya kupita lile eneo.