Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 6 Finance Wizara ya Fedha 76 2025-04-15

Name

Neema Kichiki Lugangira

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NEEMA K. LUGANGIRA aliuliza: -

Je, hatua gani zimechukuliwa kupunguza makali ya mabadiliko ya sera za nje katika masuala ya fedha za maendeleo kimataifa kwa mataifa yaliyoendelea?

Name

Dr. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Iramba Magharibi

Answer

WAZIRI WA FEDHA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge Neema Lugangira, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imekamilisha tathmini ya athari zitakazojitokeza kwa miradi ambayo ilikuwa ikipata ufadhili kupitia Serikali ya Marekani. Maeneo yaliyoathirika kwa kiasi kikubwa ni pamoja na Sekta ya Afya. Aidha, miradi mikubwa iliyokuwa inagharamiwa kupitia mshirika huyo imetengewa bajeti kupitia fedha za ndani.

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea na tathmini kwa maeneo mengine yanayoweza kuathirika kwa kiasi kikubwa kutokana na mabadiliko ya sera hizo za nje katika masuala ya fedha kwa kuangalia washirika wengine wa maendeleo ambao Serikali ya Marekani imekuwa ikitoa mchango wao.