Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Neema Kichiki Lugangira

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NEEMA K. LUGANGIRA aliuliza: - Je, hatua gani zimechukuliwa kupunguza makali ya mabadiliko ya sera za nje katika masuala ya fedha za maendeleo kimataifa kwa mataifa yaliyoendelea?

Supplementary Question 1

MHE. NEEMA K. LUGANGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu ya Serikali ninaomba kwa ufupi sana nieleze, miradi ambayo ilikuwa inafadhiliwa na Serikali ya Marekani kupitia USAID ni zaidi ya shilingi trilioni mbili, lakini pia tukiacha Serikali ya Marekani, Serikali ya Ufaransa, Serikali ya Sweden, Finland, Canada, Belgium, Netherland pamoja na EU zimetangaza kupunguza misaada. Sasa kwa kuzingatia mabadiliko haya ni dhahiri kwamba ni zaidi ya Sekta ya Afya ambayo inaweza ikaathirika: Sekta ya Elimu, Tehama, Kilimo, Mifugo na kadhalika. Kwa hiyo, nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza; kwa kuzingatia sasa hivi tuko kwenye bajeti, je, Serikali haioni iko haya ya kufanya tathmini ya kuondoa non-essential costs ili tuweze kuokoa fedha na fedha hizo zikaelekezwa kufidia hizi gap?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; ninatambua wiki ijayo Mheshimiwa Waziri ambaye ni mbobezi kabisa katika uchumi unakwenda Marekani katika mkutano wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani. Je, Serikali haioni iko haja ya ku-negotiate na Benki ya Dunia na IMF ili ile fedha ambayo tunalipa kwenye mikopo badala ya kulipa principle na interest tulipe tu principal amount, ile interest amount iwe frozen ili fedha hizo zielekezwe kwenye kufidia gap la hii athari ambayo imejitokeza? Ahsante. (Makofi)

Name

Dr. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Iramba Magharibi

Answer

WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ninampongeza Mheshimiwa Mbunge kwa maswali yake na ningekuwa na mimi natokea Kagera ningesema in fact yuko current sana. Haya anayoyaongelea ni mambo ya sasa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli tumefanya tathmini hiyo na katika tathmini hiyo tayari tumeshaanza kufanyia kazi, mapendekezo haya ya kuangalia namna ya kufanya restructuring ya matumizi ili kuweza ku-cover fedha hizo ambazo zinahitajika ni jambo ambalo tumeliweka kwenye mkakati kama Serikali na tayari tumeanza utekelezaji wake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hili ni jambo ambalo tutaendelea kulifanyia kazi kama ambavyo Serikali tayari iliunda timu ambayo ilikuwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia sekta zote na hii ambayo tumei-cite ni ile ambayo ilionekana kwamba kuna eneo linahitaji kuchukua hatua za haraka kwa sababu ni afya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu wazo la pili la kujadiliana na taasisi ambazo tuna madeni nazo, kwamba tulipe principal peke yake, ni wazo zuri, tumelipokea na tunaendelea kufanyia kazi taratibu ambazo huwa zinafanyika kwenye masuala haya ya mikopo ili kuweza kunufaika na hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utakumbuka nchi yetu iliwahi kunufaika wakati ule kwenye mpango wa EPIC, lakini hata baada ya hapo kuna taratibu ambazo huwa tunaendelea nazo zikiwemo Dedswap pamoja na maeneo mengine. Kwa hiyo, na hili nalo nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali itaufanyia kazi utaratibu huu. (Makofi)