Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 6 Community Development, Gender and Children Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum 77 2025-04-15

Name

Ussi Salum Pondeza

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chumbuni

Primary Question

MHE. ASYA SHARIF OMAR K.n.y. MHE. USSI SALUM PONDEZA aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha Taasisi zisizo za Kiserikali (NGOs) zinakuwa hai na zinaleta matokeo chanya kwa Taifa letu?

Name

Dr. Dorothy Onesphoro Gwajima

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nominated

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE NA URATIBU (MHE. UMMY H. NDERIANANGA) K.n.y. WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Serikali imechukua hatua mbalimbali za kuimarisha mazingira wezeshi ya utendaji wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali. Hatua hizo ni pamoja na:-

(a) Kuandaliwa kwa Mwongozo wa Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Tanzania Bara (2020), Toleo la Mwaka 2024, unaoelekeza vikao kazi vya robo mwaka na ushiriki wa mashirika katika vikao vya ushauri ngazi ya Kata (WDC), Tarafa, Wilaya na Mkoa;

(b) Kuandaliwa kwa Mfumo wa Kieletroniki wa Usajili na Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NIS) na Ramani ya Kidijiti ya Utambuzi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ili kurahisisha usajili, uwasilishaji wa taarifa na ulipaji wa ada;

(c) Kuanzishwa kwa Madawati ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika Wizara za Kisekta ili kuboresha uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na kuongeza ufanisi katika utendaji kazi;

(d) Kuandaliwa kwa Mkakati wa Kitaifa wa Uendelevu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali 2022 hadi 2027 ili kupunguza utegemezi na kuimarisha uendelevu wa mashirika. Mkakati huo utapelekea kuanzishwa kwa Mfuko wa Pamoja wa Ruzuku kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali; na

(e) Kushirikiana na Wasajili Wasaidizi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ngazi za Mikoa na Halmashauri. Kufanya ufuatiliaji na tathmini ya shughuli za mashirika yasiyo ya Kiserikali kwa mujibu wa Kifungu cha 4(1)(J) cha Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Sura ya 56 ya Sheria za Tanzania. Ahsante.