Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Asya Sharif Omar
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ASYA SHARIF OMAR K.n.y. MHE. USSI SALUM PONDEZA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha Taasisi zisizo za Kiserikali (NGOs) zinakuwa hai na zinaleta matokeo chanya kwa Taifa letu?
Supplementary Question 1
MHE. ASYA SHARIF OMAR: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Serikali nina swali moja la nyongeza. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuweka mazingira wezeshi ya kuzisaidia nchi iweze kupata fedha kutoka katika taasisi mbalimbali za Kikanda na Kimataifa? Ahsante sana.
Name
Ummy Hamisi Nderiananga
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE NA URATIBU (MHE. UMMY H. NDERIANANGA) K.n.y. WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninampongeza Mheshimiwa Asya kwa kazi nzuri na kwa swali lake. Kama nilivyoeleza kwenye jibu la msingi, Serikali inaendelea kufanya kazi kwa ukaribu na NGOs na kwa niaba ya Serikali niendelee kuzishukuru NGOs zote za Tanzania kwa namna ambavyo tunashirikiana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, utaona hata mikutanao mikubwa ya kimataifa ya kikanda ambayo viongozi wetu wakuu wamekuwa wakishiriki hususan Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweza kuwakutanisha wadau mbalimbali ambao wameweza kuleta fedha kwa ajili ya kusaidia sekta ya NGOs ili kuweze kuleta mchango. Tunashirikiana nao na hata tunapo-table bajeti ya Serikali tunaweka fedha za ndani na za nje. Pia, zipo NGOs Kimataifa ambazo zinapata fedha kupitia mazungumzo ya ubia ya bilateral na mengine, tunapata fedha hizo zinaingia kwenye NGO kusaidia wananchi wetu katika maeneo mbalimbali. Ahsante.
Name
Omar Ali Omar
Sex
Male
Party
ACT
Constituent
Wete
Primary Question
MHE. ASYA SHARIF OMAR K.n.y. MHE. USSI SALUM PONDEZA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha Taasisi zisizo za Kiserikali (NGOs) zinakuwa hai na zinaleta matokeo chanya kwa Taifa letu?
Supplementary Question 2
MHE. OMAR ALI OMAR: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa fursa ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri, je, Serikali ina mkakati gani wa kila mwezi kuzisaidia hizi asasi za kiraia ambazo sasa hivi zinapumulia mashine kutokana na hali zao za kiuchumi?
Name
Ummy Hamisi Nderiananga
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE NA URATIBU (MHE. UMMY H. NDERIANANGA) K.n.y. WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti, inaomba nianze kwa kumshukuru Mheshimiwa Omar kwa swali lake. Hapa nimpongeze na kumshukuru Dada yetu Mkurugenzi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Ndugu Vickness Mayao kwa kazi nzuri wanayoifanya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali tumesema tunaenda kufanya tathmini ya kina kuona namna tunaweza kusaidia. Kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi kule kwa Mheshimiwa Waziri Ridhiwani tumeanza upande wa Serikali kuzipa asasi zisizo za Kiserikali hususan mashirikika ya watu wenye ulemavu kupitia Mfuko wa Taifa wa Watu Wenye Ulemavu kuwasaidia fedha ambayo inaweza kuendelea kuwasaidia, kwa hiyo, Serikali tayari tuna mkakati huo wa kuanza
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mbunge tuendelee kushirikiana kama una mchango wa namna nzuri tunayoweza kuyasaidia mashirika haya unaweza kutuona Serikali, lakini kwa sasa tunaenda hivyo na Waziri Mama Gwajima kwenye sekta yake anafanya vizuri, anatusaidia kuona namna ya kwenda vizuri. Ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved