Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 6 Industries and Trade Wizara ya Viwanda na Biashara 78 2025-04-15

Name

Tunza Issa Malapo

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ESTHER N. MATIKO K.n.y MHE. TUNZA I. MALAPO aliuliza:-
Je, kuna mkakati gani wa kujenga viwanda vya kuchakata chumvi Mkoani Mtwara?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI WA MADINI K.n.y WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Tunza Issa Malapo kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea kutekeleza Mkakati wa Ujenzi wa Viwanda nchini ikiwemo viwanda vya chumvi. Mkakati huo unahusisha uboreshaji wa mazingira ya biashara na uwekezaji, utengenezaji wa maeneo ya biashara na viwanda na uhamasishaji wa uongezaji wa thamani kwa bidhaa/malighafi kote nchini ikiwemo Mkoa wa Mtwara.

Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia kuwa Mikoa ya Lindi na Mtwara haikuwa na Kiwanda cha Kuchakata Chumvi, Serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) inaendelea na ujenzi wa Kiwanda cha Kuchakata Chumvi Mkoani Lindi. Kiwanda hicho kitakapokamilika kitakuwa kinapokea chumvi ghafi kutoka kwa wazalishaji wadogo wakiwemo wa Mkoa wa Mtwara. Aidha, Serikali kupitia SIDO inaendelea kubuni teknolojia rahisi za kuchakata chumvi ikiwemo kusaga na kurutubisha chumvi kwa ajili ya kusaidia masuala ya lishe. Ahsante sana.