Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Esther Nicholus Matiko
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ESTHER N. MATIKO K.n.y MHE. TUNZA I. MALAPO aliuliza:- Je, kuna mkakati gani wa kujenga viwanda vya kuchakata chumvi Mkoani Mtwara?
Supplementary Question 1
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru. Nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; sote tunakubali kwamba chumvi ni kati ya bidhaa ambazo zinatumika kila siku nyumbani na kwa asilimia kubwa chumvi ambazo zinatumika Tanzania ni imported. Ninataka kujua Serikali hiki kiwanda ambacho wanajenga Lindi kina uwezo kiasi gani wa kuweza kuzalisha chumvi ambayo pia tunaweza kuuza nje ya nchi na kuongeza fedha za kigeni?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kama alivyosema Mheshimiwa Naibu Waziri pale, ni kweli kwamba sasa hivi wananchi wa Lindi na Mtwara wanauza chumvi ile kama malighafi na thamani yake ni ndogo sana. Sasa ninataka kujua ni lini kiwanda hiki kinaenda kukamilika ili kuweza kuongeza thamani ya chumvi ile na kuleta ajira kwa wananchi hao wa Mtwara na Lindi? (Makofi)
Name
Dr. Stephen Lemomo Kiruswa Mamasita
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Longido
Answer
NAIBU WAZIRI WA MADINI K.n.y. WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, ninampongeza Mheshimiwa Matiko kwa kuuliza haya maswali mawili ya nyongeza ambayo ni ya msingi sana katika kuielewa sekta ya chumvi inavyofanya kazi nchini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa swali lake la uwezo wa kiwanda kinachojengwa, ni kiwanda kidogo cha mfano ambacho Wizara ya Madini imewekeza katika kutafuta teknolojia rahisi ya kuwasaidia wawekezaji wengine wadogo nchini kuanzisha mitambo ya aina hiyo. Kwa hiyo, uwezo wake ni tani 15,000 mpaka tani 25,000 kwa mwaka. Kitakwenda kununua chumvi za wazalishaji wadogo wa chumvi na kuiongezea thamani ili iweze kuingia katika masoko ya ndani na hata nje pale ambapo watakuwa wamepata masoko ya nje.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa swali lake la pili kwamba ni lini kitakamilika. Kiwanda hiki ambacho sasa hivi kiko katika hatua za awali za ujenzi, msingi utakaobeba ile mitambo umefikia 70%. Kufikia mwezi Agosti, 2025 mitambo itakuwa imesimikwa na uzalishaji utakuwa umeanza na kiwanda hiki kitatumika kama kiwanda darasa kwa ajili ya vikundi mbalimbali na wazalishaji wa chumvi nchini kwenda kujifunza kutoka kule kabla Serikali haijaweza kuanzisha vituo vingine vya mfano sehemu mbalimbali nchini ambapo chumvi inapatikana. Ahsante sana. (Makofi)
Name
Nicodemas Henry Maganga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbogwe
Primary Question
MHE. ESTHER N. MATIKO K.n.y MHE. TUNZA I. MALAPO aliuliza:- Je, kuna mkakati gani wa kujenga viwanda vya kuchakata chumvi Mkoani Mtwara?
Supplementary Question 2
MHE. NICODEMAS H. MAGANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi. Ninaomba kumuuliza Waziri wa Viwanda na Biashara, Wilaya ya Mbogwe ina maeneo yanye viwanda lakini tuna kiwanda kimoja tu kinachofanya kazi. Ni mpango upi wa Serikali kwenye hili eneo la viwanda ili na yale maeneo tuliyoyatenga kwa ajili ya viwanda kuwawezesha wazawa ambao wanajishughulisha na shughuli zile ili waweze kukaa kwenye shughuli za viwanda?
Name
Dr. Stephen Lemomo Kiruswa Mamasita
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Longido
Answer
NAIBU WAZIRI WA MADINI K.n.y. WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyojibu kwenye majibu ya swali la msingi, Wizara ya Viwanda ina mkakati mahsusi wa kuendelea kuwekeza katika ujenzi wa viwanda katika maeneo mbalimbali nchini zinapopatikana malighafi ambazo zina warrant au zinaruhusu kuanzisha kiwanda kwa ajili ya zao au bidhaa yoyote ambayo inaweza ikachakatwa katika viwanda ambavyo Wizara hii inaendelea kuasisi.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved