Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 6 Industries and Trade Wizara ya Viwanda na Biashara 79 2025-04-15

Name

Condester Michael Sichalwe

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Momba

Primary Question

MHE. CONDESTER M. SICHALWE aliuliza:-

Je, Mitambo mingapi ya kutengeneza Gongo imesambazwa kwa wananchi wanaojishughulisha na uzalishaji wa pombe ya gongo?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer


NAIBU WAZIRI WA MADINI K.n.y. WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, mpaka sasa viwanda vya kutengeneza pombe kali nchini inayokidhi viwango, vinaendelea kuanzishwa kwa kupata mafunzo na ushauri wa kitaalam kutoka Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO), Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na miongoni mwao wako watengenezaji wanaoendelea kupata alama ya ubora kwa kukidhi vigezo.

Mheshimiwa Spika, SIDO itaendelea kushirikiana na taasisi nyingine za maendeleo ya teknolojia ikiwemo Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo (TEMDO), Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC) na kwa ushirikiano wa karibu wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS), kwa kuboresho teknolojia za kuchakata pombe kali kwa teknolojia rahisi ili watengenezaji wengi waweze kutengeneza pombe bora inayostahili kwa matumizi ya binadamu.

Mheshimiwa Spika, gongo ni pombe yenye kilevi ambayo imekuwa ikitengenezwa kienyeji. Aidha, Serikali haijahalalisha pombe ya gongo kwa sababu ya kuwa na madhara makubwa katika mwili wa binadamu. Kwa msingi huo, mpaka sasa hakuna mitambo ya kutengeneza kinywaji hicho iliyosambazwa kwa wananchi. Kwa sasa, Serikali haijaanzisha mpango wa kusambaza mitambo ya gongo kwa wananchi wanaojishughulisha na uzalishaji wa pombe ya gongo. Ahsante sana. (Makofi)