Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 6 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 80 2025-04-15

Name

Abeid Ighondo Ramadhani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Singida Kaskazini

Primary Question

MHE. ABEID R. IGHONDO aliuliza:-

Je, lini ujenzi wa Skimu ya Umwagiliaji katika Jimbo la Singida Kaskazini utaanza?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inaendelea na utekelezaji wa miradi ya umwagiliaji ambayo imefikia hatua mbalimbali. Mradi wa Skimu ya Mughamo kwa sasa upo katika hatua ya kukamilisha usanifu. Usanifu huo utakapokamilika, taratibu za kutangaza, kwa ajili ya kupata mkandarasi zitaanza mara moja. Ahsante sana.