Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Abeid Ighondo Ramadhani
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Singida Kaskazini
Primary Question
MHE. ABEID R. IGHONDO aliuliza:- Je, lini ujenzi wa Skimu ya Umwagiliaji katika Jimbo la Singida Kaskazini utaanza?
Supplementary Question 1
MHE. ABEID R. IGHONDO: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu hayo mazuri ya Serikali, ambayo naomba kasi isiongezeke, ili scheme hiyo iweze kuanza utekelezaji wake mara moja, ninayo maswali mengine mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza; ni hatua gani ambayo imefikiwa ya kuwezesha miundombinu ya umwagiliaji katika Mabwawa ya Kisisi, Masoheda, Mwahirimbi, Ntambuko, Endeshi pamoja na Mgori, ambayo niliwahi kuuliza swali la msingi hapa, kwamba, kungeanza utekelezaji, lakini mpaka sasa sijaona?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; katika Jimbo la Singida Kaskazini tuliahidiwa na Serikali kwamba, tutapatiwa visima virefu 150 vya umwagiliaji katika vijiji mbalimbali, ambavyo vina mabonde mazuri yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji, lakini mpaka sasa hakuna kinachoendelea. Je, ni hatua gani sasa ambayo Serikali inawaahidi wananchi wa Singida Kaskazini ambao walisubiri visima hivyo kwa hamu sana? Ninashukuru sana.
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimthibitishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba, katika maeneo yote ambayo ameyataja ikiwemo Kisisi, Migori najua kwamba, miradi hii ipo katika hatua mbalimbali. Moja ya wajibu wetu sisi, kama Wizara, ni kuendelea kutafuta fedha, ili kuitekeleza na mingine tunaendelea kuifanyia usanifu, ili kuhakikisha tunapata gharama halisi ya mradi, ili twende katika hatua ya mwisho ya kutafuta mkandarasi. Kwa hiyo iko katika hatua mbalimbali na ninaweza kukupa takwimu zake baadaye.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu visima 150 ni kwamba, tutatekeleza miradi hiyo kama tulivyoahidi. Sasa hivi Wizara ya Kilimo tayari tumenunua magari ya uchimbaji wa visima manne, mawili yameshafika yapo pale Wizarani na mawili yako kwenye meli, kwa ajili ya kuja hapa nchini, ambayo ni ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji. Kwa hiyo, tunataka kuhakikisha kwamba, ile ahadi ya visima 10,000 ambayo tumeahidi kupeleka katika majimbo inatekelezeka kwa vitendo. Ahsante sana. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved