Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 6 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Waziri wa Mifugo na Uvuvi 81 2025-04-15

Name

Boniphace Mwita Getere

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bunda

Primary Question

MHE. ESTER A. BULAYA K.n.y. MHE. BONIPHACE M. GETERE aliuliza:-

Je, lini Serikali itakamilisha ahadi ya ujenzi wa Mnada wa Mifugo Mngeta, Bunda?

Name

Alexander Pastory Mnyeti

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2025/2026, Serikali haikuweka kwenye mpango ujenzi wa minada mipya hapa nchini ili kutoa fursa ya ukamilishwaji wa minada 23 ya awali iliyopo katika hatua mbalimbali za ujenzi. Serikali ina jukumu la moja kwa moja la kujenga na kuendesha minada ya upili na mpakani, hivyo Wizara itaendelea kuweka katika mpango wa bajeti ujenzi wa minada ya awali nchini, ikiwemo mnada wa Mifugo Mngeta kulingana na upatikanaji wa fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, katika bajeti ya mwaka 2023/2024, Serikali ilitenga jumla ya shilingi 435,238,870, kwa ajili ya ujenzi wa mnada wa Bitalaguro uliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda. Aidha, Mwezi Februari, 2025 ujenzi wa mnada huo ulikamilika. Hivyo, kukamilika kwa ujenzi wa Mnada wa Bitalaguro utatoa fursa kwa wananchi wa Halmashauri ya Bunda kuuza na kununua mifugo katika mnada huo.