Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Ester Amos Bulaya

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ESTER A. BULAYA K.n.y. MHE. BONIPHACE M. GETERE aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha ahadi ya ujenzi wa Mnada wa Mifugo Mngeta, Bunda?

Supplementary Question 1

MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niulize maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; suala la Mnada wa Mngeta ni la muda mrefu, tunaitaka Serikali ihakikishe inatujengea Mnada wa Mngeta. Ni lini Serikali mtahakikisha mnajenga Mnada wa Mngeta?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; ni kweli, Serikali imejenga Mnada wa Bitalaguro katika Jimbo la Bunda Mjini, lakini ule mnada uko kwenye hali mbaya na mazingira ni mabovu. Je, ni lini Serikali itahakikisha inaweka mazingira rafiki ya Mradi wa Bitalaguro ili wafugaji wetu waweze kwenda kuuza mifugo yao kwenye mnada wenye staha?

Name

Alexander Pastory Mnyeti

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze na hili la kwanza, la ujenzi wa Mnada wa Mngeta. Utakumbuka kwamba, Waheshimiwa Wabunge wamekuwa wakichangia mada mbalimbali humu Bungeni na tumekwishapokea maelekezo ya Kamati yetu ya Mifugo wakielekeza kwamba, minada hii tunapoianzisha, tuhakikishe kwamba, inakamilika. Sasa hatuwezi kuwa tunaanzisha minada, tunajenga kwa 20% tunauacha, tunajenga tena mwingine, 30% tunauacha. Ndiyo maana tukasema kwanza tukamilishe miradi yote ya minada iliyoko ndani ya nchi yetu, ikishakamilika hiyo, basi ndiyo tunaweza tukaanza kujenga minada mipya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, huu wa Mngeta nimwombe sana Mheshimiwa Mbunge, kwa niaba ya Mheshimiwa Getere kwamba, asubiri tutakapokamilisha minada yote 23 tunayoijenga nchini ndipo tutaanza kujenga mnada mpya na ndiyo imekuwa ni maelekezo ya Bunge na Wabunge wengi wameshauri hivyo kwamba, tujenge minada, tukiikamilisha ndiyo tuanze minada mipya. Kwa hiyo, huu wa Mngeta tutaujenga kama tutakuwa tumekamilisha miradi yote ya maendeleo iliyopo ndani ya Wizara yetu ya Mifugo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii miundombinu ya Bitalaguro; miundombinu tutaendelea kuikarabati, tumeshajenga choo, tumeshajenga ofisi, tumejenga uzio. Kwa hiyo, tunaendelea kukarabati taratibu kadri ya upatikanaji wa fedha. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, mara fedha zinapopatikana tutapeleka kwenda kukarabati. Pia, niiombe na halmashauri, kwa sababu inapata mapato huko, iweze kukarabati katika miundombinu midogo midogo ambayo inahusiana na maeneo yao. Ahsante.

Name

Saashisha Elinikyo Mafuwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Hai

Primary Question

MHE. ESTER A. BULAYA K.n.y. MHE. BONIPHACE M. GETERE aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha ahadi ya ujenzi wa Mnada wa Mifugo Mngeta, Bunda?

Supplementary Question 2

MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, Wilaya ya Hai tulileta maombi maalum ya ukarabati wa majosho katika Kata ya Kia, Weruweru na Rundugai. Je, lini Serikali itaanza kufanya ukarabati wa majosho haya? Ahsante.

Name

Alexander Pastory Mnyeti

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli tulipokea maombi ya Mheshimiwa Mbunge na nitumie nafasi hii kumpongeza sana. Majosho haya tumeshayaingiza kwenye utaratibu, mara tutakapopata fedha tutakwenda kuyakarabati, ahsante.

Name

Edward Olelekaita Kisau

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kiteto

Primary Question

MHE. ESTER A. BULAYA K.n.y. MHE. BONIPHACE M. GETERE aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha ahadi ya ujenzi wa Mnada wa Mifugo Mngeta, Bunda?

Supplementary Question 3

MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Bajeti ya 2024/2025 walitenga pesa, shilingi milioni 500, kwa ajili ya Mnada wa Dosidosi. Ni lini mradi huu utaanza?

Name

Alexander Pastory Mnyeti

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Mwenyekiti, tunafanya mobilization ya fedha. Mara tutakapopata fedha tutakwenda kumalizia Mradi huo wa Dosidosi.