Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 7 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 82 2025-04-16

Name

Munira Mustafa Khatib

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MUNIRA MUSTAPHA KHATIB aliuliza: -

Je, Serikali ina mkakati gani wa kuongeza idadi ya madaktari na wauguzi hasa maeneo ya vijijini?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kutenga bajeti na kuajiri watumishi wa kada mbalimbali za afya nchini. Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2020/2021 – 2024/2025, jumla ya watumishi wa kada mbalimbali za afya 34,720 wameajiriwa. Wataalamu hao ni pamoja na madaktari 1,851; wauguzi 10,213 pamoja na kada nyingine 22,656. Aidha, zaidi ya 70% ya watumishi hawa wamepangiwa kazi kwenye vituo vya maeneo ya vijijini.

Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kutenga bajeti na kuajiri watumishi wa kada mbalimbali za afya na kuwapanga katika maeneo yenye upungufu hususan vijijini katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, ahsante.