Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Munira Mustafa Khatib
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MUNIRA MUSTAPHA KHATIB aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kuongeza idadi ya madaktari na wauguzi hasa maeneo ya vijijini?
Supplementary Question 1
MHE. MUNIRA MUSTAPHA KHATIB: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipatia nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kwanza ninapenda kuipongeza Serikali kwa majibu mazuri, lakini nina swali moja la nyongeza.
Mheshimiwa Spika, watumishi wengi hasa kada ya afya wanaopangiwa maeneo ya vijijini wanakuwa wanaomba uhamisho pindi tu wanapopata ajira hizo; je, Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha wanaboresha makazi kwa watumishi wa kada ya afya, hasa maeneo ya vijijini ili kuweza kuwaruhusu watumishi hawa wanapoajiriwa kubakia kwenye vituo vyao vya kazi?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ni kweli, kama alivyosema Mheshimiwa Munira Mustapha kwamba kumekuwa na changamoto ya baadhi ya watumishi wanaoajiriwa maeneo ya vijijini kuomba kuhamia maeneo ya mijini. Sasa hivi Serikali imeweka utaratibu kwanza kwa kuhakikisha kwamba tunadhibiti wimbi la uhamisho wa watumishi kutoka vijijini kwenda mijini kwa sababu wana hoja ya msingi kwamba wananchi wa vijijini pia wanahitaji kupata huduma za afya.
Mheshimiwa Spika, katika eneo hilo, moja ya hatua ambazo Serikali imechukua ni pamoja na kuboresha mazingira ya kazi ya vituo vya vijijini kwa maana ya ujenzi wa vituo bora zaidi vya kisasa, vilevile kujenga nyumba za watumishi (madakatari na wauguzi).
Mheshimiwa Spika, katika miaka hii mitatu, jumla ya nyumba 270 three in one zimejengwa ambazo zina uwezo wa kuchukua kaya 810 za watumishi wa sekta ya afya. Zoezi hili ni endelevu, hivyo tutaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kujenga nyumba za watumishi maeneo ya vijijini, ahsante.
Name
Deo Kasenyenda Sanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Makambako
Primary Question
MHE. MUNIRA MUSTAPHA KHATIB aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kuongeza idadi ya madaktari na wauguzi hasa maeneo ya vijijini?
Supplementary Question 2
MHE. DEO K. SANGA: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru kwa kuniona, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, katika Jimbo la Makambako Kituo cha Afya Lyamkena na kule Kitandililo hatuna watumishi.
Je, ni lini Serikali itapeleka watumishi ili wananchi waweze kupata huduma?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ahsante sana, Serikali imekuwa ikiajiri watumishi na kuwapeleka katika Halmashauri ya Makambako na halmashauri zote kote nchini. Kama ambavyo jibu langu la msingi linasema, katika miaka hii minne Serikali imeajiri zaidi ya watumishi 34,720 na Halmashauri ya Makambako imeendelea kupata watumishi.
Mheshimiwa Spika, ninafahamu kuwa ni kweli kwamba Kituo cha Afya cha Kitandililo na Lyamkena bado vina upungufu wa watumishi. Ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba kila kibali cha ajira kitakapotoka tutahakikisha tunapeleka watumishi katika vituo hivyo vya afya. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved