Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 7 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 83 2025-04-16

Name

Ghati Zephania Chomete

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. GHATI Z. CHOMETE aliuliza: -

Je, kwa nini katika Kituo cha Afya Iramba wanawake na watoto wanalazwa katika wodi moja?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Kituo cha Afya Iramba katika Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti kinahudumia wananchi wapatao 77,027. Serikali inatambua upungufu wa miundombinu katika vituo vya afya, hali inayopelekea baadhi ya vituo kukosa miundombinu ya msingi ikiwemo wodi za kulaza watoto, wanawake na wanaume.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2025/2026 Serikali kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti imetenga shilingi milioni 75 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa wodi ya watoto, wanawake na wanaume katika Kituo cha Afya cha Iramba.