Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Ghati Zephania Chomete

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. GHATI Z. CHOMETE aliuliza: - Je, kwa nini katika Kituo cha Afya Iramba wanawake na watoto wanalazwa katika wodi moja?

Supplementary Question 1

MHE. GHATI Z. CHOMETE: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru sana, lakini pia ninashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali. Kituo cha Afya cha Iramba ni kituo cha muda mrefu ambacho mpaka sasa miundombinu ni mibovu sana.

Mheshimiwa Spika, ninapenda kujua; je, Serikali imejipanga vipi kuhakikisha inaondoa tatizo hili la watoto na wanawake wa Kituo cha Afya cha Iramba kulala pamoja, yaani wodi moja?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, Kituo cha Afya cha Ikizu kina changamoto kama hiyo hiyo kwamba wanawake wanaosubiri kujifungua, wanawake waliojifungua na waliofanyia operation wanalala wodi moja.

Je, ni upi mkakati wa Serikali wa kuondoa tatizo hilo katika Kituo cha Afya cha Ikizu? Ahsante.

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ahsante sana, ninamhakikishia Mheshimiwa Zephania Chomete kwamba kwanza Serikali ilishafanya tathmini na kuorodhesha vituo vyote vya afya chakavu na kongwe na tayari tunakwenda kuandaa mpango mkakati wa ukarabati na upanuzi wa vituo hivyo vya afya. Katika hatua hiyo tutahakikisha pia kwamba Kituo cha Afya cha Iramba kinazingatiwa na kupewa kipaumbele. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunafahamu kwamba kuna upungufu wa wodi za wananume na wanawake. Serikali imeshaanza kuchukua hatua kwa kutenga shilingi milioni 75 katika mwaka wa fedha ujao wa fedha wa 2025/2026. Tutaanza ujenzi wa wodi hizo kupitia mapato ya ndani, lakini Serikali Kuu pia itatenga fedha kwa ajili ya kwenda kujenga wodi hizo.

Mheshimiwa Spika, suala la pili, kuhusiana na Kituo cha Afya cha Ikizu, ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kuwa suala la Kituo cha Afya cha Ikizu linafahamika na limeshawasilishwa, limewekwa kwenye Mpango wa Benki ya Dunia kwa ajili ya kwenda kukitanua na kuongeza majengo, kwa maana ya wodi za wanawake, watoto pamoja na wananume.

Name

Twaha Ally Mpembenwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kibiti

Primary Question

MHE. GHATI Z. CHOMETE aliuliza: - Je, kwa nini katika Kituo cha Afya Iramba wanawake na watoto wanalazwa katika wodi moja?

Supplementary Question 2

MHE. TWAHA A. MPEMBENWE: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru kwa kunipa nafasi kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, wapigakura wangu wa Kata ya Bungu wanataka kujua; je, ni lini Serikali itakamilisha ile ahadi ya kupeleka shilingi milioni 200 ili kuboresha miundombinu katika kituo kile cha afya?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, Kituo cha Afya cha Bungu ni moja ya vituo ambavyo vinahudumia wananchi wengi na Serikali ilishapeleka fedha kwa hatua za mwanzo. Ninamhakikishia tu Mheshimiwa Mbunge kwamba tutapeleka fedha kwa ajili ya kukitanua Kituo cha Afya cha Bungu ili kiweze kutoa huduma bora sana kwa wananchi. (Makofi)