Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 7 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 84 2025-04-16

Name

Pauline Philipo Gekul

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Babati Mjini

Primary Question

MHE. FLATEI G. MASSAY K.n.y. MHE. PAULINE P. GEKUL aliuliza:-

Je, ipi kauli ya Serikali kwa wakulima na wafanyabiashara kulipishwa crop cess zaidi ya mara moja wanapovusha mazao yao halmashauri nyingine?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ushuru wa mazao katika halmashauri hutozwa kwa mujibu wa kifungu cha 16(1)(a) na (b) (cash crops and food crops) cha Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa, Sura 290. Sheria hiyo imeweka kiwango cha asilimia tatu ambacho hutozwa kwa mazao yanayozidi tani moja yanayosafirishwa kwenda nje ya halmashauri. Aidha, ushuru wa mazao hutozwa mara moja kwa wafanyabiashara wanaonunua mazao kutoka kwa wakulima na kuyasafirsha nje ya halmashauri.

Mheshimiwa Spika, mfanyabiashara anapaswa kuwa na stakabadhi ya ushuru aliolipia muda wote wa usafirishaji wa mzigo ili kuepuka usumbufu. Baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu wamekuwa wakisafirisha mazao hayo kidogo kidogo kwa hutumia maguta, pikipiki na bajaji ili yasifikie ujazo wa tani moja ambayo hulipiwa ushuru. Wafanyabiashara hao wanapobainika hutozwa ushuru wa mazao kulingana na wingi wa mazao waliyoyasafirisha.
Mheshimiwa Spika, aidha, mamlaka zote za Serikali za Mitaa zihakikishe zinasimamia utoaji wa ushuru wa mazao kwa mujibu wa sheria.