Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Flatei Gregory Massay
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbulu Vijijini
Primary Question
MHE. FLATEI G. MASSAY K.n.y. MHE. PAULINE P. GEKUL aliuliza:- Je, ipi kauli ya Serikali kwa wakulima na wafanyabiashara kulipishwa crop cess zaidi ya mara moja wanapovusha mazao yao halmashauri nyingine?
Supplementary Question 1
MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa tabia hii imekuwa inajitokeza mara nyingi, hasa kwenye Halmashauri ya Babati Mjini na Babati Vijijini, na Halmashauri ya Mbulu, kwa sababu ziko karibu karibu na wameweka mageti: -
Je, una mpango gani wa kuwaelekeza moja kwa moja wakurugenzi ili kutotoza ushuru huu mara mbili?
Mheshimiwa Spika, swali la pili, kuna wengine wanachukua mazao shambani kuleta nyumbani: -
Je, ni nini kauli ya Serikali kuhusu hili na hawa hawasafirishi, wanapeleka ghalani (nyumbani) kama matumizi ya kawaida?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ahsante sana, kwanza nitumie nafasi hii kuwasisitiza wakurugenzi wote kote nchini, lakini hususan Wakurugenzi wa Halmashauri ya Babati Mjini, Vijijini na Mbulu pamoja na halmashauri nyingine zote za Mkoa wa Manyara wahakikishe wanatoza ushuru wa mazao kwa kufuata sheria. Wananchi wote ambao ni wakulima wanaosafirisha mazao hayo kupeleka nyumbani hawatakiwi kutozwa ushuru wa mazao, isipokuwa kwa wale ambao wanasafirisha nje ya halmashauri zaidi ya tani moja na kwa maana ya shughuli za kibiashara.
Mheshimiwa Spika, suala la pili kuhusu wananchi ambao ni wakulima katika halmashauri hizo wanafahamika, kwa hiyo, ikiwa mwananchi anasafirisha mazao yake kutoka shambani kwa maana ya ujazo wa zaidi ya tani moja kupeleka nyumbani hatakiwi kutozwa ushuru na kwa sababu viongozi wa halmashauri wa vijiji wanawafahamu wakulima hao, basi ninatumia nafasi hii kuwashauri wakulima wahakikishe wanatoa taarifa katika vijiji vyao kwamba wanasafirisha mazao hayo kupeleka nyumbani kwa maana ya kuepuka ushuru, lakini pia na changamoto nyingine, lakini nitumie nafasi hii kuwasisitiza wakurugenzi kusimamia ushuru huo kwa kufuata sheria.
Name
Yahaya Omary Massare
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Manyoni Magharibi
Primary Question
MHE. FLATEI G. MASSAY K.n.y. MHE. PAULINE P. GEKUL aliuliza:- Je, ipi kauli ya Serikali kwa wakulima na wafanyabiashara kulipishwa crop cess zaidi ya mara moja wanapovusha mazao yao halmashauri nyingine?
Supplementary Question 2
MHE. YAHAYA O. MASSARE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, utekelezaji wa sheria hii ya kukusanya ushuru katika halmashauri zetu umekuwa na changamoto kutoka eneo moja hadi eneo lingine. Je, Serikali sasa ipo tayari kuboresha kwa kutunga sheria au kuleta maboresho ya sheria hii ya cess?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, utozaji wa ushuru wa mazao crop cess upo kwa mujibu wa sheria na halmashauri zote zinalazimika na zinawajibika kufuata sheria hiyo. Tunafahamu kuna mapungufu ya baadhi ya halmashauri kutozingatia utozaji wa ushuru huu kwa mujibu wa sheria. Ninaomba nitumie nafasi hii nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, tumeshatoa maelekezo kwa Makatibu Tawala wa Mikoa, tumeshatoa maelekezo kwa wakurugenzi na wataalamu wote katika halmsahauri zetu kuhakikisha wanazingatia utozaji kwa kufuata sheria. Ofisi ya Rais, TAMISEMI itaendelea kufuatilia kwa karibu na pale ambapo utapata changamoto kwenye halmashauri Waheshimiwa Wabunge watatufikishia taarifa na wananchi ili tuweze kuchukua hatua na kudhibiti changamoto hiyo, ahsante. (Makofi)
Name
Sophia Hebron Mwakagenda
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. FLATEI G. MASSAY K.n.y. MHE. PAULINE P. GEKUL aliuliza:- Je, ipi kauli ya Serikali kwa wakulima na wafanyabiashara kulipishwa crop cess zaidi ya mara moja wanapovusha mazao yao halmashauri nyingine?
Supplementary Question 3
MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Waziri, tumehamasisha vijana kujiunga katika vikundi na kupata mikopo ya halmashauri, wapo wanaobeba ndizi kutoka Wilaya la Rungwe na kupeleka Dar es Salaam pale Mahakama ya Ndizi kuuza, lakini sheria hii inawaathiri sana na hasa pale Mikumi kwa sababu magari mengi yanasimamishwa na mazao haya yanaharibikia njiani.
Mheshimiwa Spika, mnaonaje sasa kama kuna haja ya Bunge lijalo kuweza kubadilisha sheria na hasa kwa wale tuliowashawishi kuchukua mikopo ya halmashauri, kwa sababu wanashindwa kurudisha kutokana na sheria hii?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ahsante sana, ninaomba tupokee hoja ya Mheshimiwa Mwakagenda ni hoja ya msingi na nzuri na sisi Serikali tukaifanyie tathmini kuona uwezekano wa kuiboresha au kuweka mazingira mazuri zaidi hususan kwa maeneo hayo ambayo wananchi wanasafirisha mazao kutoka halmashauri moja kwenda katika masoko makubwa Dar es Salaam na maeneo mengine.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved