Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 7 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 85 2025-04-16

Name

Rehema Juma Migilla

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Ulyankulu

Primary Question

MHE. OMARI M. KIGUA K.n.y. MHE. REHEMA J. MIGILLA aliuliza:-

Je, lini Serikali itafanya ukarabati wa Shule za Msingi Taba, Mkindo, Kaswa, Mbeta na Milambo?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, mwaka 2024/2025 Serikali ilitoa shilingi milioni 380 kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya Shule za Msingi za Seleli, Makingi, Ntyemo, Kagunga, Kabanga, Unampanda na Kashishi za Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua. Katika mpango na bajeti ya mwaka 2025/2026 Serikali inatarajia kutumia shilingi milioni 270 kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya shule za msingi 10 zikiwemo Shule za Milambo, Ichemba, Kaswa, Mbeta, Taba na Mkindo. Serikali itaendelea kutenga fedha ya ukarabati wa miundombinu ya shule chakavu zikiwemo Shule za Msingi Taba, Mkindo na Milambo kadiri ya upatikanaji wa fedha.