Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Omari Mohamed Kigua
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilindi
Primary Question
MHE. OMARI M. KIGUA K.n.y. MHE. REHEMA J. MIGILLA aliuliza:- Je, lini Serikali itafanya ukarabati wa Shule za Msingi Taba, Mkindo, Kaswa, Mbeta na Milambo?
Supplementary Question 1
MHE. OMARI M. KIGUA: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Rehema, niipongeze Serikali kwa majibu na matumaini makubwa kwa wananchi wa Ulyankulu lakini pamoja na hayo ni kwamba Shule ya Msingi Mkindi katika Jimbo hilo la Ulyankulu ni kwamba mvua iliyonyesha tarehe 10 Aprili, iliezua madarasa matano. Je, nini mpango mkakati wa kuhakikisha kwamba madarasa yale yanarejeshwa katika hali ya kawaida?
Mheshimiwa Spika, swali la pili, Shule ya Msingi Masagalu katika Wilaya ya Kilindi ni shule yenye historia kubwa ambayo ilijengwa mwaka 1948 ikiwa ni middle school, lakini shule ile imechakaa, nini mpango mkakati wa kuikarabati shule ile? Ahsante. (Makofi)
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, ni kweli tarehe 10 Aprili, 2025 mvua na upepo mkali uliezua madarasa matano katika Shule ya Msingi ya Mkindu. Kwa kweli Mheshimiwa Rehema Migilla amekuwa akifanya ufuatiliaji wa hali ya juu kuhakikisha kwamba zinachukuliwa hatua kwa ajili ya kurejesha miundombinu katika shule hizo ili pale shule zitakaporejea wanafunzi waweze kutumia madarasa haya matano.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba nitumie nafasi hii kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI kumwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua kuchukua hatua za dharura kutumia mapato ya ndani kwenda kurekebisha madarasa hayo matano ili madarasa hayo yaweze kutumika pindi shule zitakapofunguliwa.
Mheshimiwa Spika, kuhusiana na swali la pili la Mheshimiwa Mbunge kuhusiana na shule chakavu katika Jimbo lake la Kilindi, ninaomba niendelee kutoa taarifa kwamba Serikali ya Awamu ya Sita katika kipindi cha miaka minne imefanya uwekezaji wa zaidi ya shilingi trilioni 5.1 katika sekta ya elimu msingi na sekondari. Katika kipindi cha miaka hiyo shule 832 chakavu za msingi zimekarabatiwa.
Kwa hiyo, ninaomba nitumie nafasi hii kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali itaendelea na jitihada hizo na itafika katika shule hii katika Jimbo lako kwa ajili ya kuhakikisha inafanyiwa ukarabati ili iweze kuwa katika hadhi nzuri na wanafunzi wetu wapate sehemu nzuri ya kusoma.
Name
Jonas Van Zeeland
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mvomero
Primary Question
MHE. OMARI M. KIGUA K.n.y. MHE. REHEMA J. MIGILLA aliuliza:- Je, lini Serikali itafanya ukarabati wa Shule za Msingi Taba, Mkindo, Kaswa, Mbeta na Milambo?
Supplementary Question 2
MHE. JONAS V. ZEELAND: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, Shule ya Msingi Mnyanza, Shule ya Msingi Mbogo, Masalaka, Mvomero, Kisimagulu, Kichangani, Kikeo na Melela hizi ni shule kongwe sana na zina madarasa chakavu sana...
SPIKA: Swali.
MHE. JONAS V. ZEELAND: Mheshimiwa Spika, je, Serikali ina mkakati gani sasa kutenga fedha kwa ajili ya kuzikarabati na kuongeza vyumba vipya vya madarasa?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, nianze kwanza kwa kumpongeza Mheshimiwa Mbunge kwa swali hili ambalo nia yake ni kuhakikisha miundombinu katika shule hizi za msingi inaweza kuboreshwa.
Mheshimiwa Spika, ninaomba nitumie nafasi hii kuendelea kuwakumbusha Wakurugenzi wa Halmashauri kufanya tathmini katika shule hizi chakavu na kuweka katika mpango na bajeti na kwa kuanzia kwenye mapato ya ndani ili shule hizi ziweze kufikiwa na kufanyiwa ukarabati. Kwa hiyo, kwa nafasi hii ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali itafika katika shule hizi chakavu ili iweze kuzirekebisha na ziwasaidie wanafunzi wetu.
Name
Samweli Xaday Hhayuma
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Hanang'
Primary Question
MHE. OMARI M. KIGUA K.n.y. MHE. REHEMA J. MIGILLA aliuliza:- Je, lini Serikali itafanya ukarabati wa Shule za Msingi Taba, Mkindo, Kaswa, Mbeta na Milambo?
Supplementary Question 3
MHE. SAMWELI X. HHAYUMA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.
Mheshimiwa Spika, je, ni lini Serikali itapeleka fedha Shule ya Msingi Bassodesh ambayo ni shule maalumu kwa watoto wa wafugaji na ni shule ya bweni ila majengo yake yaweze kukarabatiwa?
Name
Yussuf Kaiza Makame
Sex
Male
Party
CUF
Constituent
Chake Chake
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, Serikali ya Awamu ya Sita katika kipindi cha miaka minne imefanya uwekezaji mkubwa wa zaidi shilingi trilioni 5.1 katika upande wa kuboresha elimu msingi na elimu sekondari. Ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge dhamira ya Serikali ni kufika katika shule nyingi zaidi kuziboresha kwa ajili ya kuhakikisha watoto wetu wanapata maeneo mazuri ya kujifunzia na walimu pia wanapata maeneo mazuri ya kufundishia. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge Serikali itafika katika shule alizozitaja katika jimbo lake kwa ajili ya kuhakikisha zinakarabatiwa na zinakuwa katika hadhi nzuri.
Name
Shabani Omari Shekilindi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Lushoto
Primary Question
MHE. OMARI M. KIGUA K.n.y. MHE. REHEMA J. MIGILLA aliuliza:- Je, lini Serikali itafanya ukarabati wa Shule za Msingi Taba, Mkindo, Kaswa, Mbeta na Milambo?
Supplementary Question 4
MHE. SHABANI O. SHEKILINDI: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru, je, ni lini Serikali itapeleka pesa za ukarabati katika Shule ya Msingi Makanya pamoja na Shule ya Msingi Kwayi maana shule hizi zimechoka na ni za zamani mno tangu mkoloni?
Mheshimiwa Spika, ninaomba majibu kwa Mheshimiwa Naibu Waziri.
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Shekilindi kwamba katika kipindi cha miaka minne shule za msingi chakavu 832 zimefikiwa. Nimhakikishie kuwa Serikali tayari imeshaanza kuzifikia shule hizi chakavu na itaendelea kufikia shule nyingi zaidi. Nimhakikishie kwamba na yeye katika jimbo lake Serikali itafika kwa ajili ya kufanya ukarabati katika shule alizozitaja.