Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 7 Good Governance Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) 87 2025-04-16

Name

Dr. Alice Karungi Kaijage

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. ALICE K. KAIJAGE aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kufuatilia waajiri ili wawe wanatoa mafunzo kwa watumishi kabla ya kustaafu?

Name

Deus Clement Sangu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwela

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Serikali imetoa maelekezo kwa waajiri kupitia Kanuni G.1(7) ya Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma za mwaka 2009, kuhakikisha wanaandaa mipango ya mafunzo kwa watumishi na kufanya tathmini ya mahitaji ya mafunzo (training need assessment), kutenga bajeti na kusimamia utekelezaji wake. Katika kutekeleza maelekezo hayo, kwa kipindi cha mwaka 2022/2023 hadi mwaka 2024/2025, jumla ya watumishi 3,036 kutoka kwa waajiri mbalimbali walipatiwa mafunzo kabla ya kustaafu katika Chuo cha Utumishi wa Umma. Hata hivyo, Serikali itaendelea kuwasisitiza waajiri kuhakikisha suala la mafunzo kwa watumishi kabla ya kustaafu linapewa kipaumbele katika utumishi wa umma, ninakushukuru.