Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Dr. Alice Karungi Kaijage
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. ALICE K. KAIJAGE aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kufuatilia waajiri ili wawe wanatoa mafunzo kwa watumishi kabla ya kustaafu?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. ALICE K. KAIJAGE: Mheshimiwa Spika, ahsante, pamoja na majibu mazuri ya Serikali nilikuwa na maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, je, Serikali haioni sasa kuna haja ya kuhusisha mifuko ya hifadhi ya jamii hata kutoa elimu kwa wastaafu watarajiwa kwa sababu wanasema wanatoa kwa muda mfupi na kwao unaona haina tija, kwa hiyo hili pengine ni gharama hii mifuko inayohifadhi fedha zao kwa nini isihusishwe ikawa muhusika mkuu wa kutoa elimu kwa hawa wastaafu watarajiwa kwa kipindi cha kutosha?
Mheshimiwa Spika, swali la pili, je, Serikali ina mpango gani kutoa upendeleo kwa wastaafu ili kupata uwekezaji katika hatifungani za BOT kama ilivyo kwa baadhi ya taasisi chache? (Makofi)
Name
Deus Clement Sangu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kwela
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru sana, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Dkt. Alice kwa namna anavyofuatilia masuala ya watumishi.
Mheshimiwa Spika, nikijibu maswali mawili ya nyongeza, ameuliza ni namna gani Serikali tuna mpango wa kuihusisha mifuko ya jamii katika kutoa elimu ya wastaafu kabla hawajastaafu.
Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge jambo hili tumeliweka kwenye utekelezaji na taasisi za waajiri zimeanza sasa kuweka mpango wa kushirikiana na mifuko hii ya hifadhi ya jamii kutoa elimu. Pia tunahakikisha sasa tumetoa maelekezo kama Serikali, elimu hii inatolewa mapema kwa sababu wengine wamekuwa wakitoa elimu hiyo kwa wastaafu mwezi mmoja kabla ya kustaafu ambayo inakuwa haiwasaidii, sasa tumejipanga kutoa elimu hii mapema ili kumpa nafasi mstaafu anapostaafu anakuwa tayari anajua afanye nini baada ya kumaliza utumishi wake wa umma.
Mheshimiwa Spika, juu ya kuwekeza kwenye hatifungani; Serikali pamoja na elimu ambayo tumesisitiza kutoa kwa wastaafu ni kuwekeza kwenye hatifungani kwa maana ni sehemu ambapo risk yake ni ndogo. Kupitia mfuko wetu wa UTT AMIS tumeanzisha product ya Wekeza Bond kwa maana ya Bond Fund ambayo inatoa masharti nafuu kabisa na ambayo inamwezesha mstaafu kupata gawio lake kila mwezi.
Mheshimiwa Spika, ninashukuru sana. (Makofi)
Name
Dr. Angeline Sylvester Lubala Mabula
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Ilemela
Primary Question
MHE. DKT. ALICE K. KAIJAGE aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kufuatilia waajiri ili wawe wanatoa mafunzo kwa watumishi kabla ya kustaafu?
Supplementary Question 2
MHE. DKT. ANGELINE S. L. MABULA: Mheshimiwa Spika, ahsante, pamoja na mpango mzuri wa Serikali ambao upo kwa ajili ya watumishi wanaotarajia kustaafu sasa; je, ni nini hatua ya Serikali kwa wale ambao walistaafu zamani na hawakuwa na bahati ya kupata haya mafunzo, lakini bado wanadai mafao yao hawajayapata wakiwemo wale waliokuwa watumishi wa East Africa? (Makofi)
Name
Deus Clement Sangu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kwela
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru na ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Mabula, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, ni kweli kuna baadhi ya wastaafu ambao hawakupata faida ya mafunzo haya, lakini kama Serikali tumeweka mkakati na mwingine, bado wanaendelea kudai mafao haya. Tutakapokuwa tunashughulikia masuala hayo tutahakikisha pia tunaongea na waajiri wao wa zamani kuhakikisha wanapewa mafunzo ili tutakapokamilisha kuwalipa fedha hizi waende kuwekeza mahali ambapo patakuwa na tija zaidi na kutokuwaacha stranded. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved