Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 7 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 89 2025-04-16

Name

Joseph George Kakunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sikonge

Primary Question

MHE. JOSEPH G. KAKUNDA aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itawezesha wakulima wasio na fedha taslimu kupata mikopo ya mbolea ya ruzuku?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante sana, kwa sasa Serikali inatoa ruzuku ya mbolea kwa wakulima ambapo mkulima huchangia gharama wakati wa ununuzi. Kwa mwaka wa fedha 2024/2025 tani 388,619.8 za mbolea zenye thamani ya ruzuku ya shilingi bilioni 131.66 imeuzwa kwa utaratibu huo.

Mheshimiwa Spika, Serikali inafanya tathmini ya namna ya kutoa ruzuku ya mbolea kwa njia ya mkopo ili kuwawezesha wakulima wasio na fedha taslimu kupata mbolea hiyo. Wakati tunakamilisha tathmini hiyo, tunashauri wakulima ambao hawana fedha taslimu kujiunga na Vyama vya Ushirika (AMCOS au SACCOS) ili waweze kukopa pembejeo kupitia vyama hivyo. Aidha, wakulima hao pia wanaweza kupata mikopo ya riba nafuu kupitia Benki ya Maendeleo ya Ushirika, Mfuko wa Pembejeo za Kilimo (AGITF) na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB).