Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Joseph George Kakunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sikonge

Primary Question

MHE. JOSEPH G. KAKUNDA aliuliza: - Je, ni lini Serikali itawezesha wakulima wasio na fedha taslimu kupata mikopo ya mbolea ya ruzuku?

Supplementary Question 1

MHE. JOSEPH G. KAKUNDA: Mheshimiwa Spika, kwanza, ninafurahi sana kwa majibu ya Serikali hasa wanaposema wanaandaa tathmini, lakini nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza; je, Serikali ipo tayari kuandaa na kutoa mwongozo pamoja na elimu itakayowezesha wakulima kupata mikopo kwenye hizi Benki za Ushirika na Benki ya Wakulima (TADB) kwa sababu wakulima wengi hawana habari na hawajui utaratibu wa kufikia kupata mikopo hiyo?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; mikopo ya Mfuko wa Pembejeo za Kilimo imekuwa ikichelewa sana tangu mwombaji aombe wakati mwingine inachukua hata miaka miwili; je, Serikali haioni kwamba hatua hizo zinakatisha tamaa wakulima?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, mimi nimpongeze Mheshimiwa Mbunge na nimthibitishie tu kwamba Serikali ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ni makini sana katika kumsaidia mkulima. Tutakuwa tayari kuendelea kutoa mwongozo kwa mkulima wa kuzisisitiza hizi taasisi ambazo tunazisimamia ziweze kuongeza elimu maana yake waongeze bajeti ili waweze kuwafikia watu wengi. Kwa hiyo, tutalifanya hivyo ili tuweze kuwafikia wakulima kama ambavyo umeshauri.

Mheshimiwa Spika, hukusu mikopo ya Mfuko wa Pembejeo (AGITF) kuendelea kuchelewa, nitoe tu maelekezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa AGITF kwamba ahakikishe mikopo wanaitoa kwa haraka. Sisi kama Wizara moja ya wajibu wetu ni kufuatilia kuona mikopo hiyo inawafikia wakulima kwa sababu fedha hiyo tunayo. (Makofi)

Name

Justin Lazaro Nyamoga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilolo

Primary Question

MHE. JOSEPH G. KAKUNDA aliuliza: - Je, ni lini Serikali itawezesha wakulima wasio na fedha taslimu kupata mikopo ya mbolea ya ruzuku?

Supplementary Question 2

MHE. JUSTIN L. NYAMOGA: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru; kwenye kilimo cha mazao ya mboga mboga hasa nyanya, viazi, vitunguu na mazao mengine yanayofanana, tatizo kubwa ni viuatilifu yaani dawa zinazotumika ambazo ni gharama kubwa sana.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuweka ruzuku kwenye viuatilifu hivyo ili wakulima hao pia wapate nafuu katika shughuli zao za kilimo? (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, ninakubaliana na pendekezo la Mheshimiwa Nyamoga, lakini sasa hivi sisi kama Serikali tunatekeleza huu mpango wa ruzuku kwa awamu na ndiyo maana unaona tumefanya kwenye mbolea, kwenye upande wa mazao kwa mfano ya chakula kama mahindi na tunafanya viuatilifu kwenye mazao ya biashara kama vile korosho.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ni mpango endelevu ambao tumekuwa tukifanya. Kwa hiyo, tunakwenda hatua kwa hatua tukiangalia changamoto zinazojitokeza ili tuhakikishe sasa baadaye tutawafikia na hao. Kwa hiyo, jambo hilo tumelipokea na tutalifanyika kazi.

Name

Mohamed Lujuo Monni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chemba

Primary Question

MHE. JOSEPH G. KAKUNDA aliuliza: - Je, ni lini Serikali itawezesha wakulima wasio na fedha taslimu kupata mikopo ya mbolea ya ruzuku?

Supplementary Question 3

MHE. MOHAMED L. MONNI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, kuna ucheleweshaji mkubwa wa pembejeo hasa mbolea za ruzuku pamoja na mbegu katika Jimbo zima la Chemba, ninataka kujua kauli ya Serikali juu ya ucheleweshaji huo, ahsante.

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, niseme tu kwamba sisi kama Serikali, kama kuna kipindi tumejitahidi kupeleka mbolea kwa wakati ninafikiri katika msimu huu uliopita hususani mbolea za kawaida kwa wakulima. Baada ya kutambua zile changamoto zilizojitokeza katika msimu uliopita mwaka huu tutaongeza idadi ya mawakala kwa ajili ya kusambaza pembejeo. Vilevile kutumia vyama vya ushirika ili kuhakikisha mbolea za ruzuku zinawafikia wakulima. Kwa hiyo, tutalizingatia hilo hususani katika Jimbo lako la Chemba. (Makofi)