Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 7 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 90 2025-04-16

Name

Mwantatu Mbarak Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

House of Representatives

Primary Question

MHE. MWANTATU MBARAK KHAMIS aliuliza: -

Je, Serikali imewezaje kutatua changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo (ASDP I)?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante sana, changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Kwanza (ASDP I) ni pamoja na miundombinu duni ya kilimo kwa maana ya barabara, maghala na miundombinu ya umwagiliaji; upatikanaji mdogo wa pembejeo kama mbegu bora, mbolea na viuatilifu; huduma duni za ugani; ushirikishwaji mdogo wa sekta binafsi; na upungufu wa takwimu sahihi za kilimo.

Mheshimiwa Spika, kutokana na hali hiyo, Serikali imezingatia katika kutatua changamoto hizo kupitia mipango inayoendelea kutekelezwa ukiwemo Mpango wa Muda Mrefu wa Mageuzi ya Sekta ya Kilimo kwa maana ya Tanzania Agricultural Master Plan - 2050. Maeneo ya kipaumbele yanayoendelea kutekelezwa kwa sasa ni kuendelea kuwekeza kwa kuimarisha upatikanaji wa pembejeo za kilimo, huduma za ugani, utafiti, uzalishaji wa mbegu, kuongeza uwezo wa kuhifadhi mazao, upatikanaji wa masoko, kuimarisha upatikanaji wa takwimu na kuhamasisha uwekezaji wa sekta binafsi ambao ulikuwa wa chini wakati wa utekelezaji wa ASDP I.