Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Mwantatu Mbarak Khamis
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
House of Representatives
Primary Question
MHE. MWANTATU MBARAK KHAMIS aliuliza: - Je, Serikali imewezaje kutatua changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo (ASDP I)?
Supplementary Question 1
MHE. MWANTATU MBARAK KHAMIS: Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa nimpongeze Mheshimiwa Waziri kwa majibu yake, lakini kwa kuzingatia changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa programu hii; je, katika mipango inayoendelea mmejipanga vipi katika suala zima la kuboresha, kuratibu, kufuatilia pamoja na kufanya tathmini ili kuhakikisha mafanikio ya programu hii yanapatikana kwa lengo la kuboresha sekta ya kilimo nchini? (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, mimi pia nimpongeze Mheshimiwa Mwantatu kwani amekuwa ni mfuatiliaji mzuri sana wa jambo hili.
Mheshimiwa Spika, ni kweli sisi kama Wizara sasa hivi tumeandaa Kitengo cha M and E kwa ajili ya kuhakikisha inafuatilia mipango yote ambayo inatekelezwa katika Wizara yetu. Kwa hiyo, tunataka ufuatiliaji pamoja na utekelezaji wake uende kama vile ambavyo Serikali imepanga na kukusudia. Kwa hiyo, tutaongeza nguvu pamoja na bajeti kuhakikisha yale yote tuliyokusudia yanatekelezeka. Kwa hiyo, nimshukuru sana Mheshimiwa Mbunge kwa hilo. (Makofi)
Name
Cecilia Daniel Paresso
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MWANTATU MBARAK KHAMIS aliuliza: - Je, Serikali imewezaje kutatua changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo (ASDP I)?
Supplementary Question 2
MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali dogo la nyongeza.
Mheshimiwa Spika, pamaja na umuhimu wa sekta ya kilimo, inakabiliwa na changamoto nyingi lakini changamoto hizo tunaweza kupunguza kama tukianzisha Mfuko wa Kilimo na ukiwa na vyanzo vya uhakika. Nini kauli ya Serikali kuanzisha mfuko huu? (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, ni kwamba tayari tumeshaanzisha Mfuko wa Kilimo ambao tunaita Mfuko wa Pembejeo za Kilimo. Moja ya jukumu kubwa tulilonalo sasa hivi ni kuendelea kuuongezea fedha na bahati nzuri tulishapata grants kwa ajili ya mfuko huo karibu dola milioni 15. Kwa hiyo, tutaendelea kuongeza fedha ambazo zitawafanikisha kuwafikia wakulima wengi. Kwa hiyo, tupo katika utekelezaji.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved