Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 7 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Waziri wa Mifugo na Uvuvi 91 2025-04-16

Name

Joseph Zacharius Kamonga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ludewa

Primary Question

MHE. DEODATUS P. MWANYIKA K.n.y. MHE. JOSEPH Z. KAMONGA aliuliza: -

Je, kuna mpango gani wa kupeleka meli ya Uvuvi Ziwa Nyasa ili kuvua samaki wanaoishi kwenye kina kirefu ambao kwa sasa wanakufa kwa uzee?

Name

Alexander Pastory Mnyeti

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Serikali kwa sasa ina mpango wa kununua meli kwa ajili ya uvuvi wa Bahari Kuu. Vilevile Serikali imeweka msukumo mkubwa kwenye ununuzi wa boti za kisasa kwa ajili ya kuvua kwenye maziwa yote nchini ambapo kwa mwaka 2022/2023 Wizara imefanikiwa kupeleka Ziwa Nyasa boti nne za kisasa pamoja na zana za kuvulia samaki.

Mheshimiwa Spika, boti zilizopelekwa Ziwa Nyasa zina urefu wa mita 7.06, mita 10 na mita 12. Kati ya boti hizo nne, boti mbili zenye urefu wa mita 10 na ile ya mita 12 zina uwezo wa kuvua kwenye kina kirefu cha Ziwa Nyasa. Boti hizo zilitolewa kupitia ushirikiano baina ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kupitia mikopo isiyo na riba kwa vikundi vya wavuvi, makampuni, vyama vya wavuvi, vyama vya ushirika na mtu mmoja mmoja.

Mheshimiwa Spika, boti hizo nne zilizopelekwa Ziwa Nyasa kwa mwaka wa fedha 2022/2023 zilitolewa kwa Kyela Education Improvement Foundation (Kyela), Christopher N. Ndunguru (Nyasa), Hubbert Authur Wayotile (Ludewa) na Godfred Raphael Mwasoka (Ludewa). Aidha, utoaji wa boti hizo ni endelevu hivyo Wizara inahamasisha wavuvi na vikundi vya wavuvi kuendelea kuomba mikopo hiyo ili waweze kunufaika na fursa hiyo, ahsante. (Makofi)