Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Deodatus Philip Mwanyika
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Njombe Mjini
Primary Question
MHE. DEODATUS P. MWANYIKA K.n.y. MHE. JOSEPH Z. KAMONGA aliuliza: - Je, kuna mpango gani wa kupeleka meli ya Uvuvi Ziwa Nyasa ili kuvua samaki wanaoishi kwenye kina kirefu ambao kwa sasa wanakufa kwa uzee?
Supplementary Question 1
MHE. DEODATUS P. MWANYIKA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana na ninashukuru sana kwa majibu mazuri na tunawashukuru sana Serikali kwa mpango huo wa boti ambao tayari zimeshaanza kupelekwa kule, lakini nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, swali la kwanza; tunafahamu wazi kwamba tija kubwa inatokana hasa na boti, lakini kuwa na vizimba. Ni lini Serikali itapeleka vizimba ili viweze kuwasaidia vijana waweze kuvua kwa urahisi katika Ziwa Nyasa? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali la pili; Halmashauri ya Mji Njombe haina kituo ambacho kingetumika kama shamba darasa kwa ajili ya kutunza vifaranga na kufanya multiplication. Ni lini sasa Serikali itatengeneza au itaweka mpango wa kuwa na shamba darasa kwa ajili ya Halmashauri ya Mji Njombe? (Makofi)
Name
Alexander Pastory Mnyeti
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Misungwi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika, ni kweli kwa Ziwa Nyasa bado Serikali haijaweka utaratibu maalumu kuhusiana na vizimba kwa sababu tayari imeshaanza utafiti wa namna gani na wapi ambako vizimba vinaweza vikawekwa katika Ziwa letu Nyasa na tayari tumeshakamilisha utafiti huo juu ya kujua wapi tunaweza tukaweka vizimba ili vitakapoenda vizimba hivyo viwe na tija kwa wafugaji wetu wa samaki katika eneo hilo.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tumeshakamilisha utafiti huo na baada ya utafiti huo basi sasa tutakwenda kutoa semina kwa wavuvi wetu juu ya wapi panafaa kuwekwa vizimba katika Ziwa Nyasa. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tayari tumeshakamilisha utafiti na baada ya hapo tutatuma wataalamu kwa ajili ya kutoa elimu juu ya vizimba, lakini na wapi ambapo vizimba vinaweza vikafaa.
Mheshimiwa Spika, kuhusiana na shamba darasa tumelipokea hili la Mheshimiwa Mbunge kwamba tutakwenda kuwafundisha wavuvi wetu wa eneo hilo. Tutakwenda kuweka shamba darasa kwa ajili ya kuendelea kufanya demonstration kwa wavuvi wetu katika eneo hilo. Ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tumelichukua na tutakwenda kulifanyia kazi ili tuweze kuweka tija katika eneo. (Makofi)
Name
Philipo Augustino Mulugo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Songwe
Primary Question
MHE. DEODATUS P. MWANYIKA K.n.y. MHE. JOSEPH Z. KAMONGA aliuliza: - Je, kuna mpango gani wa kupeleka meli ya Uvuvi Ziwa Nyasa ili kuvua samaki wanaoishi kwenye kina kirefu ambao kwa sasa wanakufa kwa uzee?
Supplementary Question 2
MHE. PHILLIPO A. MULUGO: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru sana kwa kunipa nafasi.
Mheshimiwa Spika, Ziwa Rukwa ni ziwa kubwa sana toka limepimwa mwaka 1978 na Serikali ilipandikiza samaki aina ya Singida enzi hizo tukiwa watoto wadogo kabisa, lakini mpaka leo samaki wa Ziwa Rukwa wamedumaa kabisa. Serikali ina mpango gani wa kupandikiza samaki wengine kwa ajili ya kuleta ustawi wa Ziwa Rukwa? (Makofi)
Name
Alexander Pastory Mnyeti
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Misungwi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika, wazo la Mheshimiwa Mbunge tunaomba tukalifanyie kazi, tutatuma wataalamu waende kuhakikisha na kuangalia kama kweli samaki wamedumaa katika Ziwa hilo halafu tuone tunaweza kufanya nini ili kuweza kunusuru samaki katika ziwa hilo, ahsante. (Makofi)
Name
Ally Anyigulile Jumbe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kyela
Primary Question
MHE. DEODATUS P. MWANYIKA K.n.y. MHE. JOSEPH Z. KAMONGA aliuliza: - Je, kuna mpango gani wa kupeleka meli ya Uvuvi Ziwa Nyasa ili kuvua samaki wanaoishi kwenye kina kirefu ambao kwa sasa wanakufa kwa uzee?
Supplementary Question 3
MHE. ALLY A. J. M. JUMBE: Mheshimiwa Spika, mmoja wa wanufaika wa mpango wa maboti ya kuvulia yupo Kyela, lakini tangu amepewa boti hilo, vifaa vyote havijakamilika na ni miaka miwili sasa. Kazi yake anayofanya ni kusafirisha abiria; je, ni lini sasa Serikali itampelekea vifaa vyote ili aweze hata kulipa mkopo wake kwa kuvua samaki? (Makofi)
Name
Alexander Pastory Mnyeti
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Misungwi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika, wakati tunatoa vifaa hivi boti pamoja na vifaa vyake vilikuwa vimekamilika, labda kama kuna tatizo la mmoja mmoja hilo ni jambo lingine. Tupo tayari kukutana na Mheshimiwa Mbunge na huyo mvuvi ili tuone namna ya kwenda kumtatulia tatizo lake. (Makofi)
Name
Ester Amos Bulaya
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DEODATUS P. MWANYIKA K.n.y. MHE. JOSEPH Z. KAMONGA aliuliza: - Je, kuna mpango gani wa kupeleka meli ya Uvuvi Ziwa Nyasa ili kuvua samaki wanaoishi kwenye kina kirefu ambao kwa sasa wanakufa kwa uzee?
Supplementary Question 4
MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Spika, ninashukuru.
Mheshimiwa Spika, wavuvi wa Bunda Mjini wamejiunga kwenye vikundi hasa wa eneo la Tahiro na Guta, lakini mpaka sasa hivi hawajapata boti ambayo itawawezesha kuvua kisasa. Ni lini sasa na wenyewe watapatiwa? (Makofi)
Name
Alexander Pastory Mnyeti
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Misungwi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema kwamba Mheshimiwa Rais alishazindua ugawaji wa boti hizi na vifaa vyake. Tupo tayari kupeleka pale Bunda kama tutapata maombi maalumu. Nafikiri baada ya Bunge hili nikutane na Mheshimiwa Mbunge anipe vikundi hivyo ambavyo vinahitaji boti na vifaa vya uvuvi ili tuweze kupewa mkopo huo kwa sababu vifaa vipo na tayari Mheshimiwa Rais amesharuhusu vigawiwe katika maeneo mbalimbali. (Makofi)
Name
Charles Muguta Kajege
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mwibara
Primary Question
MHE. DEODATUS P. MWANYIKA K.n.y. MHE. JOSEPH Z. KAMONGA aliuliza: - Je, kuna mpango gani wa kupeleka meli ya Uvuvi Ziwa Nyasa ili kuvua samaki wanaoishi kwenye kina kirefu ambao kwa sasa wanakufa kwa uzee?
Supplementary Question 5
MHE. CHARLES M. KAJEGE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru, wavuvi wa Mwibara wamechoka kufukuzana na samaki majini; je, ni lini watapatiwa vizimba ili waweze kuvua samaki wengi? (Makofi)
Name
Alexander Pastory Mnyeti
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Misungwi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika, tunaendelea na ugawaji wa vizimba katika maeneo mbalimbali na hata sasa tumeshaanza ugawaji wa vizimba awamu ya pili, tunamhakikishia Mheshimiwa Mbunge tutakwenda kugawa vizimba katika vikundi vyake vya Mwibara, bahati nzuri tumeshawasiliana na Mheshimiwa Mbunge kwa mara nyingi zaidi kwamba tumeshamwelekeza namna sahihi ya kufanya ili tuweze kwenda kugawa vizimba katika Jimbo lake, ahsante. (Makofi)