Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 7 Finance and Planning Wizara ya Fedha 92 2025-04-16

Name

Katani Ahmadi Katani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tandahimba

Primary Question

MHE. CECILIA D. PARESSO K.n.y. MHE. KATANI A. KATANI aliuliza: -

Je, lini Serikali itarejesha fedha za miradi iliyochukuliwa na Hazina ili miradi hiyo iweze kukamilishwa?

Name

Dr. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Iramba Magharibi

Answer

WAZIRI WA FEDHA alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa kifungu cha 29 cha Sheria ya Bajeti, Sura 439, fedha ambazo hazijatumika hadi mwisho wa mwaka zinakoma matumizi yake mwisho wa mwaka unapofika. Lengo kuu la kanuni hiyo ni kusimamia uwajibikaji na uwazi katika matumizi ya fedha zilizotengwa katika bajeti.

Mheshimiwa Spika, hivyo, iwapo kuna miradi ama shughuli ambayo haijakamilika, Fungu husika linatakiwa kutenga bajeti na kuwasilisha maombi kwa kuambatisha hati za madai au nyaraka za utekelezaji wa miradi hiyo.

Mheshimiwa Spika, azma ya Serikali ni kuhakikisha kuwa miradi yote inatekelezwa ili kuleta maendeleo kwa wananchi.