Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Cecilia Daniel Paresso

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. CECILIA D. PARESSO K.n.y. MHE. KATANI A. KATANI aliuliza: - Je, lini Serikali itarejesha fedha za miradi iliyochukuliwa na Hazina ili miradi hiyo iweze kukamilishwa?

Supplementary Question 1

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi na naomba kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, imekuwa ni utamaduni sasa kila inapofika mwisho wa mwaka wa Serikali ndiyo fedha nyingi sana zinaanza kutoka kiasi ambacho kinafanya inakuwa carried forward miaka mingine, lakini pia wakati mwingine ndiyo mwanya wa matumizi mabaya ya fedha.

Je, kwa nini Serikali isijipange vizuri fedha ziwe zinatoka kila awamu bila kukaribia mwisho wa mwaka? (Makofi)

Name

Dr. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Iramba Magharibi

Answer

WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, tunapokea ushauri, ni ushauri mzuri. Mara nyingi ambacho huwa kinasababisha ni pale ambapo bajeti inapopitishwa kunakuwa na taratibu za kuweza kukamilisha masuala ya manunuzi ili miradi ianze kutekelezwa na fedha zianze kupelekwa kwa ajili ya kulipia miradi hiyo, lakini miradi ambayo huwa inakuwa tayari ipo kwenye utekelezaji mara tu baada ya mwaka wa fedha kuanza, huendelea kupata fedha. Kwa hiyo, kwa ile ambayo imechelewa kuanza shughuli zake za utekelezaji mara nyingi fedha hufuatia baada ya hapo.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo wazo lililotolewa na Mheshimiwa Mbunge ni wazo la msingi na Serikali tutaendelea kuzingatia utoaji wa fedha kwa kila awamu ili kuweza kuhakikisha fedha zinazotengwa ndani ya mwaka husika zinatumika. (Makofi)

Name

Saashisha Elinikyo Mafuwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Hai

Primary Question

MHE. CECILIA D. PARESSO K.n.y. MHE. KATANI A. KATANI aliuliza: - Je, lini Serikali itarejesha fedha za miradi iliyochukuliwa na Hazina ili miradi hiyo iweze kukamilishwa?

Supplementary Question 2

MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Spika, Serikali ina mpango gani wa kupeleka fedha ili kwenda kuwalipa wakandarasi wanaojenga barabara kwa kiwango cha changarawe na lami kupitia TARURA na TANROADS ili miradi iendelee?

Name

Dr. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Iramba Magharibi

Answer

WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kutoa fedha zinazotakiwa kwenda kutekeleza miradi ya barabara ambazo Mheshimiwa Mbunge amezitaja kupitia TARURA na TANROADS, tunavyoongea katika wiki mbili hadi mwezi mmoja tumepeleka fedha kwa ajili ya TARURA na kwa ajili ya TANROADS kwa ajili ya kuendelea kutekeleza miradi ambayo wakandarasi wapo site na wanatakiwa wapate fedha ili waendelee na utekelezaji wa miradi.