Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 7 Health and Social Welfare Wizara ya Afya 93 2025-04-16

Name

Aysharose Ndogholi Mattembe

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. RITTA E. KABATI K.n.y. MHE. AYSHAROSE N. MATTEMBE aliuliza: -

Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Mradi wa Hospitali ya Mkoa Singida unatekelezwa kwa awamu ambapo hadi sasa Serikali imeshatoa fedha kiasi cha shilingi bilioni 9.3 ambapo awamu ya kwanza zilitolewa shilingi bilioni sita na awamu ya pili shilingi bilioni 3.3.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2024/2025 Serikali imetenga fedha kiasi cha shilingi bilioni nne kwa ajili za ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Singida ikiwa ni awamu ya III (Phase III). Ujenzi huu unatarajia kukamilika ifikapo mwezi Januari, 2027.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha. (Makofi)