Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Ritta Enespher Kabati

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. RITTA E. KABATI K.n.y. MHE. AYSHAROSE N. MATTEMBE aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana na ninamshukuru sana Mheshimiwa Waziri kwa majibu yake.

Je, katika ujenzi huo wa hospitali ya rufaa, Serikali imeweza kuweka na maeneo kwa ajili ya nyumba za madaktari wa hospitali hiyo, kwa sababu imekuwa ni changamoto kwenye hospitali nyingi?

Swali langu la pili, Hospitali ya Mkoa wa Iringa madaktari wanapata shida sana kwa sababu hawana nyumba za kuishi na mara nyingi madaktari wamekuwa wakipata shida kwenda kuhudumia wagonjwa wa dharura inapotokea.

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwenye mpango huu wa shilingi bilioni nne zinazokwenda, mkakati wa nyumba za madaktari umewekwa, lakini siyo mkakati tu wa nyumba za madaktari, pia vyumba vya kupumzikia madaktari wakati wanasubiri kama kutatokea dharura. Kitakachofanywa kule Singida ndicho kitakachotokea upande wa mkoa wa Hospitali ya Iringa. (Makofi)

Name

Asha Abdullah Juma

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. RITTA E. KABATI K.n.y. MHE. AYSHAROSE N. MATTEMBE aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida?

Supplementary Question 2

MHE. ASHA ABDULLAH JUMA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Hivi Serikali inaweza kulieleza Bunge hili kwa zile hospitali za rufaa ambazo zimekamilika ni zote zimepata vifaa muhimu vya hospitali ya rufaa kama MRI, scanners, x-rays, mortuary za kisasa na kadhalika?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, hospitali zote za rufaa ambazo zimekamilika ambazo ni hospitali za mikoa kwenda Taifa zimepata vifaa kulingana na level ya hospitali yenyewe na mahitaji kwa wakati huo, kwa maana ya capacity ya wataalamu waliopo site na kila wakati uhitaji unapoibuka zinaongezwa. Kwa sasa kwa maana ya mashine kama MRI ambayo umeisema hapa hiyo haipo kwenye hospitali za mikoa, utaikuta kwenye hospitali za kanda na Taifa na kwenye hospitali za mikoa utakuta CT-Scan.

Name

Condester Michael Sichalwe

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Momba

Primary Question

MHE. DKT. RITTA E. KABATI K.n.y. MHE. AYSHAROSE N. MATTEMBE aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida?

Supplementary Question 3

MHE. CONDESTER M. SICHALWE: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa kunipatia nafasi.

Mheshimiwa Spika, tunaishukuru sana Serikali kwa kutujengea hospitali yetu ya Mkoa wa Sogwe; je, ni lini mtatujengea wodi za jumla kwa ajili ya kulaza wagonjwa kwa sababu kuna upungufu mkubwa?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, nimtoe Mheshimiwa Mbunge wasiwasi, miezi mitatu iliyopita nilikuwepo kwenye Hospitali ya Mkoa wa Songwe, hospitali hiyo kwa majengo yaliyopo na vitanda bado wala wagonjwa hawajaweza kujaza, lakini ni kweli huo, wing inahitajika kwenye Hospitali yako ya Mkoa wa Songwe na kwenye bajeti ya mwaka huu ni mojawapo ya mipango inayopagwa kwa ajili ya kujenga wing hiyo, lakini kwa uhakika kwamba wagonjwa watapata shida au vitanda havitatosha kwa majengo yaliyopo bado vitanda ni vingi kuliko wagonjwa.