Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 7 Health and Social Welfare Wizara ya Afya 94 2025-04-16

Name

Nancy Hassan Nyalusi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SYLVIA F. SIGULA K.n.y. MHE. NANCY H. NYALUSI aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kumaliza tatizo la udumavu nchini?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA alijibu: -

Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana na tatizo la udumavu nchini Serikali inatekeleza mpango kazi jumuishi wa masuala ya lishe wa mwaka 2021/2022 – 2025/2026 ambapo baadhi ya afua zinazotekelezwa ni kama ifuatavyo:-

(i) Uhamasishaji na umuhimu wa ulishaji sahihi wa watoto ikiwemo unyonyeshaji.

(ii) Utoaji wa elimu ya lishe katika vituo vya afya na uhamasishaji wa jamii kupitia vyombo vya habari.

(iii) Kwa wajawazito na wazazi/walezi wanapohudhuria kliniki.

(iv) Utoaji wa matone ya Vitamini A na dawa za minyoo kwa watoto wa umri wa chini ya miaka mitano.

(v) Uongezwaji wa virutubishi (madini na vitamini) katika vyakula hasa mafuta ya kula, unga wa ngano, unga wa mahindi na chumvi.

(vi) Utoaji wa vidonge vya madini chuma na asidi ya foliki kwa wanawake wajawazito.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.