Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Sylivia Francis Sigula

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SYLVIA F. SIGULA K.n.y. MHE. NANCY H. NYALUSI aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kumaliza tatizo la udumavu nchini?

Supplementary Question 1

MHE. SYLVIA F. SIGULA: Mheshimiwa Spika, ahsante, pamoja na majibu mazuri ya Serikali nina maswali mawili ya nyongeza.

Swali la kwanza, kutoka kwenye ripoti ya Serikali mikoa inayoongoza kwa uzalishaji wa chakula ndiyo mikoa inayoongoza kwa udumavu, ikiwemo Iringa, Rukwa, Katavi pamoja na Ruvuma. Je, Serikali haioni kuna haja sasa ya kufanya utafiti ili kujua pamoja na uzalishaji huo changamoto ni nini suala la udumavu lipo juu? (Makofi)

Swali la pili, mikoa hii ambayo nimeitaja ni mikoa ambayo ina idadi kubwa ya watu; je, Serikali haioni haja ya kuja na mkakati maalumu wa kupambana na changamoto ya udumavu katika mikoa hii niliyoitaja? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, ahsante, kwanza ninampongeza Mheshimiwa Mbunge kwa swali lake hili, lakini niseme tu, Serikali imeshafanya utafiti na kilichoonekana, moja ni kweli kwamba mikoa hii inazalisha chakula, lakini ni asilimia tisa tu ya watu wanakula chakula mchanganyiko, kwa hiyo, maana yake asilimia nyingine yote inakula chakula cha aina moja. Unakuta mtu anaweza akatengeneza makande halafu yakawekwa, yakaliwa kwa muda mrefu kidogo badala ya kula vyakula vingine.

Mheshimiwa Spika, pia unakuta ule ulishaji kwenye yale makuzi ya watoto mwanzo wanapozaliwa, kuanzia kulisha ujauzito, mama mjamzito anavyolishwa, lakini pia wakati mtoto akiwa mchanga mpaka anafikisha miaka mitano, maeneo hayo kuna matatizo. Kwa hiyo, sasa hivi nguvu zimeelekezwa kwenye kubadilisha hiyo tabia.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili niseme tu kwamba pia kuhusu kutoa hamasa kwa jamii na idadi ya watu. Kwa kweli nguvu sasa hivi imeelekezwa na Serikali, lakini na mashirika mbalimbali na utaona kwenye Mkoa wa Njombe, ninampongeza Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mheshimiwa Mtaka amefanya kazi nzuri sana. Wakati wa siku ya afya juzi Mkoa wa Njombe ndiyo uliongoza karibu kila kitu katika kufanya vizuri, wakati mkoa huu kwa masuala haya ya udumavu unashika namba mbili ukiongozwa na Mkoa wa Iringa, maana yake hii mikoa sasa imeanza kuongeza nguvu kwenye masuala ya afya na masuala mbalimbali na tunaamini baada ya muda mtaona mabadiliko makubwa. (Makofi)

Name

Felista Deogratius Njau

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SYLVIA F. SIGULA K.n.y. MHE. NANCY H. NYALUSI aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kumaliza tatizo la udumavu nchini?

Supplementary Question 2

MHE. FELISTA D. NJAU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, SUA wanazalisha wataalamu wa lishe wengi sana lakini mtaani hawapo, hawajaajiriwa. Ni nini mkakati wa Serikali kuhakikisha kila kijiji, kila kata kunakuwa na mtaalamu wa lishe ili kuepuka adha ya udumavu? Ahsante. (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer


NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, ni kweli SUA wanazalisha wataalamu wa aina mbalimbali na wazuri sana na ambao wanafikiri vizuri sana kisayansi, lakini kuna mambo ambayo tunatakiwa tujadiliane na wenzetu wa Wizara ya Utumishi, baadhi wengine kwenye muundo hawapo, lakini wengine ni kwamba kuna vibali vinavyotoka tutaendelea kuwaajiri wale ambao wapo kwenye muundo, lakini wale ambao inaonekana kwenye muundo hawapo ili waweze kuingia na waweze kusaidia kutatua hayo matatizo. (Makofi)

Name

Shally Josepha Raymond

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SYLVIA F. SIGULA K.n.y. MHE. NANCY H. NYALUSI aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kumaliza tatizo la udumavu nchini?

Supplementary Question 3

MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, kwa kuwa ni miaka 64 sasa baada ya uhuru na bado tatizo hili ni kubwa.

Je, Serikali haioni kwamba ni muhimu kila hospitali ikawa na kitengo cha lishe wakati akina mama wanapoenda kliniki wakaweza kupata huduma hiyo endelevu? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwa sasa kitengo cha lishe kwenye hospitali zetu kimeanza, ukienda kwenye Hospitali za Mikoa, Taifa utakuta Afisa Lishe, tutaendelea kuongeza nguvu na utaona hata kila Wilaya kuna Afisa Lishe lengo ni kuhakikisha hayo mambo yanafanyika. Kikubwa ninachosema ni kwamba tutaongeza nguvu kuhakikisha pia lishe ni sehemu ya mtu anatoka kabisa kama anakwenda kwa daktari anaingia chumba na anamsikiliza daktari kabla ya kuondoka hospitalini. Tumeanza kila mama anapoingia kliniki wakati wa kliniki lishe ni jambo ambalo ni lazima lizungumziwe kabla ya mama kuondoka kiliniki. Tunalichukua hilo iwe ni kitu ambacho kabla haujaondoka hospitali basi uwe umemwona Afisa Lishe na muongee mambo mbalimbali.

Name

Anatropia Lwehikila Theonest

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SYLVIA F. SIGULA K.n.y. MHE. NANCY H. NYALUSI aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kumaliza tatizo la udumavu nchini?

Supplementary Question 4

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru, kwa kuwa suala la upatikanaji wa chakula shuleni limebaki kuwa suala la hiari. Kuna maeneo mengine wazazi wasipochangia watoto hawapati chakula na huo ndiyo mwanzo wa udumavu kwa sababu hawapati chakula kwa wakati.

Ni nini mkakati wa Serikali kuhakikisha chakula kinapatikana mashuleni na pale ambapo wazazi hawawezi kuchangia Serikali iweze kuhusika kusaidia upatikanaji wa chakula mashuleni?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRII WA AFYA: Mheshimiwa Spika, moja ni suala tu la kuhamasishana kwamba unapozungumzia suala la lishe huzungumzii suala la lishe tu pale mtoto anapokuwa ameanza shule, ni toka mama anapobeba ujauzito na ndipo unapopata mtoto mwenye GB za kutosha na mwenye uwezo mzuri wa akili na mwenye uwezo wa kupambana. Kila mzazi anahitaji mwanae aweze kupambana na masuala mbalimbali baadaye maishani na hata Taifa letu liweze ku-compete na mataifa mengine katika arena ya sayansi na ugunduzi.

Mheshimiwa Spika, sasa suala la kula, kama mtoto wako ameondoka nyumbani chakula cha mchana kile ambacho angekula mchana ukampelekea shuleni sioni kwamba ni tatizo. Wilaya ya Siha tumekubaliana, mtoto angekula nyumbani mchana, hicho chakula chake cha mchana kinahamishiwa tu shuleni na wazazi wamekubali wote na hakuna tatizo la lishe mashuleni. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, ninalipokea suala lako kwamba pamoja na kuhamasisha wananchi kwamba lazima tuchangie chakula shuleni, lakini pia panapotokea matatizo basi tutashauriana na Wizara ya Elimu tuone way forward, lakini ukweli ni kwamba siyo sawa ukashindwa kuhakikisha mtoto wako anakula shuleni kwa sababu mchana angekuwa nyumbani ungemlisha chakula. (Makofi)

Name

Neema Kichiki Lugangira

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SYLVIA F. SIGULA K.n.y. MHE. NANCY H. NYALUSI aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kumaliza tatizo la udumavu nchini?

Supplementary Question 5

MHE. NEEMA K. LUGANGIRA: Mheshimiwa Spika, ninashukuru kwa kunipa nafasi; kwa kuwa bado udumavu ni changamoto kubwa hapa nchini kwetu, kwa kurejea kwamba Mheshimiwa Naibu Waziri umesema kwamba Serikali inatekeleza ule mpango jumuishi wa lishe, Shirika la Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) limekuwa likifanya kazi kubwa katika eneo hili.
SPIKA: Uliza swali Mheshimiwa.

MHE. NEEMA K. LUGANGIRA: Mheshimiwa Spika, je, Wizara ya Afya haioni ipo haja ya hii Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC) kuendelea kuwepo badala ya vile Serikali ilivyoamua kuifuta? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwanza nimuondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge, TFNC haijafutwa, lakini imeboreshwa ili iweze kutenda vizuri zaidi na kuweza kutenda kwa namna ambayo inaweza kusimamiwa kirahisi zaidi. Sasa TFNC inaenda kuwa idara kamili na itasimamiwa vizuri sana na kuhakikisha inatekeleza majukumu yake kwa usahihi zaidi. (Makofi)