Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 7 Health and Social Welfare Wizara ya Afya 95 2025-04-16

Name

Lucy John Sabu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. LUCY J. SABU aliuliza: -

Je, kuna mpango gani wa kuongeza vituo vya ushauri na programu za uhamasishaji ili kusaidia vijana na tatizo la afya ya akili?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Serikali inatekeleza mikakati mbalimbali katika kupambana na tatizo la afya ya akili kama ifuatavyo: -

(i) Serikali inatoa huduma ya ushauri nasaha wa afya ya akili na uhamasishaji katika vituo vya afya 701 na hospitali zote za rufaa za mikoa pamoja na Hospitali ya Afya ya Akili Mirembe.

(ii) Serikali imefanya mafunzo kwa wataalamu 2,840 wakiwemo madaktari na wauguzi ili kuwawezesha kutambua na kushughulikia changamoto za magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo afya ya akili.

(iii) Serikali imeanzisha huduma ya call centre 115 ambapo pamoja na huduma nyingine, jamii inapata huduma ya ushauri nasaha ya afya ya akili kwa njia ya simu, lengo likiwa ni kuwafikia vijana wengi zaidi, kuwasaidia kwa haraka na pia kupunguza unyanyapaa kwa wale wasiopenda kwenda hospitalini moja kwa moja.

(iv) Serikali imeanzisha vituo 1561 vya kutoa huduma rafiki kwa vijana katika mikoa yote, ikiwemo huduma za afya ya akili kupitia Mkakati Jumuishi wa Vijana (NAIA).

Mheshimiwa Spika, ninaomba kuwasilisha. (Makofi)