Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Lucy John Sabu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. LUCY J. SABU aliuliza: - Je, kuna mpango gani wa kuongeza vituo vya ushauri na programu za uhamasishaji ili kusaidia vijana na tatizo la afya ya akili?

Supplementary Question 1

MHE. LUCY J. SABU: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina swali moja dogo la nyongeza. Kumekuwepo na changamoto kubwa kwa vijana ambao wamekosa ajira, hivyo kusababisha kuwa na msongo wa mawazo na afya ya akili. Je, Serikali ina mpango gani wa kuzuia tatizo la afya ya akili kabla kijana hajakumbwa na changamoto hiyo? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa, vilevile Serikali inatumia gharama kubwa katika kuwahudumia vijana hawa. Je, Serikali ina mpango gani sasa wa kuhakikisha kwamba changamoto hii inakwisha kabisa? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, matatizo ya akili yanayosababishwa na ukosefu wa ajira, ninafikiri tunaweza tukayakabili. Moja, kwa kuelemishana namna sahihi ya kufikiri na kuyatazama maisha. Ndiyo maana Serikali imekuja na mtaala mpya wa kuyarekebisha masuala ya elimu, ili mtu toka akiwa mtoto, chekechea, basi ajitambue na ajue kwamba, unaposoma hata usipoajiriwa kuna namna nyingine ya kufanya ukaweza kuzalisha na ukaishi.