Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 21 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 262 2025-05-09

Name

Atupele Fredy Mwakibete

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busokelo

Primary Question

MHE. ORAN M. NJEZA K.n.y. MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE aliuliza: -

Je, lini Serikali itatoa fedha kukamilisha ujenzi wa Vituo vya Afya Mpata, Isange na Ntaba – Busokelo?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer


NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kukamilisha ujenzi wa Vituo vya Afya vya Mpata, Isange na Ntaba jumla ya shilingi milioni 491 zinahitajika. Kituo cha Afya Mpata kinahitaji shilingi milioni 395, Kituo cha Afya Isange shilingi milioni 76 na Kituo cha Afya Ntaba shilingi milioni 20.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2024/2025 Serikali imetoa shilingi milioni 150 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Vituo vya Afya vya Mpata, Isange na Ntaba katika Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kukamilisha miradi viporo ya vituo vya afya nchini ikiwa ni pamoja na Vituo vya Afya vya Mpata, Isange na Ntaba, ahsante.