Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Oran Manase Njeza
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbeya Vijijini
Primary Question
MHE. ORAN M. NJEZA K.n.y. MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE aliuliza: - Je, lini Serikali itatoa fedha kukamilisha ujenzi wa Vituo vya Afya Mpata, Isange na Ntaba – Busokelo?
Supplementary Question 1
MHE. ORAN M. NJEZA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana na nashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali.
Kwa kuwa Serikali imetenga na mahitaji makubwa kwa vituo hivyo ni majengo ya OPD pamoja na upasuaji. Je, ni lini Serikali itapeleka fedha kwa ajili ya kukamilisha majengo hayo?
Swali la pili, kwa kuwa wananchi wa Kata za Ilungu, Iwindi pamoja na Kata ya Ulenje wameshajenga vituo vya afya kwa hatua kubwa. Je, ni lini Serikali itapeleka fedha kwa ajili ya kukamilisha majengo hayo ambayo yamejengwa kwa nguvu za wananchi?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, kwanza nianze kwa kuwapongeza wananchi wa Jimbo la Busokelo kwa namna ambavyo wamekuwa wakishiriki katika kuchangia nguvu zao katika ujenzi wa vituo vya afya na Serikali hii ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kutenga fedha na kuwapelekea fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo hivi vya afya, lakini tunafahamu kwamba ujenzi wa vituo hivi unakwenda kwa awamu. Serikali imeshapeleka fedha katika vituo hivi vitatu na tunafahamu kuna majengo ambayo bado yanahitajika, yakiwepo majengo ya OPD na jengo la upasuaji.
Mheshimiwa Mwenyekiti naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa Jimbo la Busekelo kwamba Serikali inafahamu na imeshaingiza kwenye mpango wa vituo vinavyohitaji fedha kwa ajili ya umaliziaji na tutahakikisha tunapeleka fedha kwa ajili ya kukamilisha vituo hivi vya afya ikiwemo ujenzi wa majengo ya OPD, jengo la upasuaji na majengo mengine ambayo yanapungua.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili niwapongeze wananchi wa Jimbo la Mbeya Vijijini ma Mheshimiwa Mbunge, kwa namna ambavyo wamejenga vituo hivyo vya afya, lakini nimhakikishie tu kwamba tayari Serikali ilishaweka utaratibu madhubuti wa kutambua vituo vya afya vyote ambavyo vimejengwa kwa nguvu za wananchi, lakini zahanati na kutenga bajeti kwa awamu kwa ajili ya kukamilisha vituo hivyo.
Kwa hiyo, Mheshimiwa Oran Njeza, nikuhakikishie tu kwamba tunafahamu na tunatenga fedha kwa ajili ya ukamilishaji wa vituo hivyo vya afya. (Makofi)
Name
Asia Abdulkarim Halamga
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ORAN M. NJEZA K.n.y. MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE aliuliza: - Je, lini Serikali itatoa fedha kukamilisha ujenzi wa Vituo vya Afya Mpata, Isange na Ntaba – Busokelo?
Supplementary Question 2
MHE. ASIA A. HALAMGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Nichukue nafasi hii kuipongeza Serikali kwa kuendelea kufanya kazi kubwa ya kuendelea kuweka fedha kwa ajili ya miundombinu ya afya.
Je, ni lini Serikali itakamilisha miundombinu katika vituo vya afya; Kituo cha Afya Endasak, Nangwa, Gisambalang pamoja na Masqaroda Jimbo la Hanang? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kwanza ilishatambua kata za kimkakati katika Jimbo la Hanang na ilikwisha peleka fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya, lakini tunafahamu kwamba vipo vituo vya afya ambavyo havijakamilika kama ambavyo Mheshimiwa Asia Halamga amesema; Kituo cha Afya cha Nangwa, Gisambalang, Endasak na Masqaroda. Nikuhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba tayari vimeshaingizwa kwenye mpango kwa ajili ya kuingizwa kwenye bajeti kwa awamu, kwa ajili ya kukamilisha vituo hivyo ili vitoe huduma bora zaidi kwa wananchi. (Makofi)
Name
Sylivia Francis Sigula
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ORAN M. NJEZA K.n.y. MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE aliuliza: - Je, lini Serikali itatoa fedha kukamilisha ujenzi wa Vituo vya Afya Mpata, Isange na Ntaba – Busokelo?
Supplementary Question 3
MHE. SYLVIA F. SIGULA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Tanzania aliahidi shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kasanga Wilaya ya Kalambo, shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa kituo pamoja na gari la wagonjwa, lakini tangu mwaka 2020 mpaka leo hatujapata fedha hizo. Je, nini kauli ya Serikali katika kutimiza ahadi hiyo ya Mheshimiwa Waziri Mkuu? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, kwanza nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Ofisi ya Rais, TAMISEMI na Serikali kwa ujumla moja ya vipaumbele ambavyo vinawekwa kwenye mipango ya utekelezaji ni ahadi na maelekezo ya viongozi wa kitaifa na tunafahamu kwamba Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliahidi kituo cha afya na tayari tumeshakiingiza kwenye mpango wa Benki ya Dunia na wakati wowote kituo hiko cha afya kitajengwa katika halmashauri ya Kalambo, ahsante. (Makofi)
Name
Boniphace Nyangindu Butondo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kishapu
Primary Question
MHE. ORAN M. NJEZA K.n.y. MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE aliuliza: - Je, lini Serikali itatoa fedha kukamilisha ujenzi wa Vituo vya Afya Mpata, Isange na Ntaba – Busokelo?
Supplementary Question 4
MHE. BONIPHACE N. BUTONDO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana, wananchi wa Kata ya Sekebugolo wameanzisha Kituo cha Afya cha Dulisi ambapo OPD ndio imekuwa ikitumika, wameanza kwa hatua ya awali. Je, Serikali ni lini itafanya ukamilishaji wa kituo kile ili kiwe na hadhi maalumu? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni dhahiri kwamba Jimbo la Kishapu kwa Mheshimiwa Butondo ni moja ya majimbo ambayo Serikali imeendelea kupeleka fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya, lakini Serikali pia ilishatoa maelekezo kwa Wakurugenzi wa Halmashauri kutenga fedha za mapato ya ndani kwa kushirikiana na nguvu za wananchi kwa ajili ya kuanza ujenzi wa vituo na Serikali itapeleka fedha kwa ajili ya kukamilisha vituo hivyo, wataalamu na vifaatiba pamoja na madawa.
Naomba nikuhakikishie Mheshimiwa Buntondo kwamba tunafahamu na tayari tumeingiza kwenye mpango na tutatafuta fedha kwa ajili ya kukamilisha kituo hicho cha afya ili tuweze kutoa huduma bora kwa wananchi. (Makofi)
Name
Innocent Sebba Bilakwate
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kyerwa
Primary Question
MHE. ORAN M. NJEZA K.n.y. MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE aliuliza: - Je, lini Serikali itatoa fedha kukamilisha ujenzi wa Vituo vya Afya Mpata, Isange na Ntaba – Busokelo?
Supplementary Question 5
MHE. INNOCENT S. BILAKWATE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Kituo cha afya Rutunguru na Kituo cha Afya Mabila ni lini Serikali itapeleka fedha ili kiweze kutumika kwa huduma zote? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi na ukamilishaji wa vituo vya afya unafanyika kwa awamu na nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba Jimbo la Kyerwa litapelekewa fedha kwa awamu kwa ajili ya kukamilisha vituo hivyo vya afya, lakini pia maboma ya zahanati kwa kadiri ambavyo ameyawasilisha.
Name
Esther Lukago Midimu
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ORAN M. NJEZA K.n.y. MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE aliuliza: - Je, lini Serikali itatoa fedha kukamilisha ujenzi wa Vituo vya Afya Mpata, Isange na Ntaba – Busokelo?
Supplementary Question 6
MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali la nyongeza.
Kwanza niishukuru Serikali kwa kuendelea kujenga vituo vya afya maeneo mbalimbali. Je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya Mwasai, Wilaya ya Maswa? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa bahati nzuri nishatembelea kata ile ya Mwasai na niliona kazi nzuri ya ujenzi ambayo Serikali ishapeleka fedha kwa ajili ya ujenzi wa Kituo kile cha Afya cha Mwasai katika Halmashauri ya Maswa na nimuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba zoezi hilo ni endelevu, tutaendelea kutenga fedha kwa awamu na kukamilisha miundombinu yote ambayo inabaki ili tuhakikishe kituo kile kinakuwa na majengo yote muhimu kwa ajili ya huduma hizo. (Makofi)
Name
Dr. John Danielson Pallangyo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Arumeru-Mashariki
Primary Question
MHE. ORAN M. NJEZA K.n.y. MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE aliuliza: - Je, lini Serikali itatoa fedha kukamilisha ujenzi wa Vituo vya Afya Mpata, Isange na Ntaba – Busokelo?
Supplementary Question 7
MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kuniona.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ilituahidi kutujengea vituo vitatu vya kimkakati na katika vile tulipata kimoja kile cha Mareu, tunasema ahsante kwa ajili ya hicho kituo, lakini sasa kuna hivi vituo vingine viwili vilivyobaki sijui vilienda wapi Mheshimiwa Waziri? Ahsante sana.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ya Awamu ya Sita na Mheshimiwa Rais wetu, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kusogeza sana huduma za afya karibu na wananchi kwa kutambua kata zote za kimkakati na kupeleka fedha na hivi karibuni Waheshimiwa Wabunge ni mashahidi tulikuwa na ahadi ya muda mrefu ya Serikali ya kuleta vituo vya afya kwa kila jimbo, tumeanza na majimbo 120 na nafahamu jimbo la Mheshimiwa Dkt. Pallangyo pia limo.
Kwa hiyo, katika vituo hivyo vya afya vitatu tayari kimoja kimeshapelekewa fedha, kimoja kitapelekewa fedha hivi karibuni lakini na hicho kingine ni kuhakikishie Mheshimiwa Dkt. Pallangyo na wananchi wa Jimbo la Arumeru kwamba fedha hiyo itapelekwa kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa vituo hivyo vya afya.