Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 21 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 263 2025-05-09

Name

Ndaisaba George Ruhoro

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ngara

Primary Question

MHE. NDAISABA G. RUHORO aliuliza: -

Je, lini Serikali itaanza kuwawezesha Maafisa Ugani kwa kuwapa mafuta ili waweze kutembelea wakulima?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua majukumu muhimu yanayofanywa na Maafisa Ugani katika kutekeleza majukumu yao kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa. Ili kuwawezesha Maafisa Ugani kutekeleza majukumu yao katika halmashauri, Serikali kupitia Wizara ya Kilimo mpaka kufikia Machi, 2025 imewapatia wataalamu hao vitendea kazi mbalimbali zikiwemo pikipiki 6,444, vishikwambi 5,426, sare 6,456 na magari 40.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2025/2026 jumla ya mikoa mitano, halmashauri 12 zimetenga bajeti ya mafuta kati ya lita 10 hadi 15 kwa kila mwezi kwa ajili ya kuwawezesha Maafisa Ugani kutekeleza majukumu yao. Serikali kupitia mapato ya ndani ya halmashauri zitaendelea kutenga bajeti ya fedha kwa ajili ya mafuta na matengenezo ya pikipiki za Maafisa Ugani ili waweze kutekeleza majukumu yao na kuongeza mapato ya ndani ya halmashauri husika, ahsante.