Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Ndaisaba George Ruhoro

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ngara

Primary Question

MHE. NDAISABA G. RUHORO aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza kuwawezesha Maafisa Ugani kwa kuwapa mafuta ili waweze kutembelea wakulima?

Supplementary Question 1

MHE. NDAISABA G. RUHORO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana, pamoja na majibu mazuri sana ya Serikali, ambapo kwa kweli tunaona Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan imeupiga mwingi kwenye eneo hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali haioni kwamba ni wakati muafaka wa kutenga mfuko maalumu kwa ajili ya maafisa ugani nchini, ili uweze kutumika kuwawezesha kupata mafuta na posho nyingine wanazozihitaji wakiwemo Maafisa Ugani wa Ngara ili waendeleze kazi nzuri ambayo ndio uti wa mgongo wa Taifa letu hasa kazi ya kilimo? Ahsante. (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer


NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza Serikali inatambua sana kazi nzuri na kubwa inayofanywa na Maafisa Ugani katika kutoa elimu, kusimamia shughuli za Kilimo na kukutana na wananchi mara kwa mara ili kuhakikisha kwamba tunaboresha shughuli za kilimo katika nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nitumie nafasi hii nimuhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba wazo alilolitoa la kuwa na mfuko maalumu kwa ajili ya Maafisa Ugani, sisi Ofisi ya Rais, TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na Serikali kwa ujumla tumelichukua kama pendekezo, tutalifanyia tathmini na kuona kama linatekelezeka kwa utaratibu gani na kama kuna maboresho mengine mbadala basi Serikali itaendelea kufanya hivyo, ahsante.