Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 21 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 264 2025-05-09

Name

Dr. Angeline Sylvester Lubala Mabula

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Ilemela

Primary Question

MHE. SHALLY J. RAYMOND K.n.y. MHE. DKT. ANGELINE S. L. MABULA aliuliza: -

Je, lini Serikali itajenga uzio katika Shule za msingi ambazo hazina uzio maeneo ya mijini?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeendelea kuboresha miundombinu ya elimu nchini ikiwa ni pamoja na kujenga uzio katika shule mbalimbali za msingi kwa kuzipa kipaumbele shule zenye watoto wenye mahitaji maalumu. Katika mwaka 2022/2023 na 2023/2024 Serikali imetoa shilingi bilioni 5.57 kwa ajili ya ujenzi wa uzio katika shule 185 za watoto wenye mahitaji maalumu. Vilevile, Mamlaka za Serikali za Mitaa zimekuwa zikitenga fedha kupitia mapato ya ndani kujenga uzio ili kuimarisha ulinzi katika maeneo yenye changamoto za kiusalama. Serikali kupitia mapato ya ndani ya halmashauri itaendelea kutenga fedha za ujenzi wa uzio kwa ajili ya usalama wa wanafunzi na mali za shule kadiri ya upatikanaji wa fedha, ahsante.