Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Shally Josepha Raymond
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SHALLY J. RAYMOND K.n.y. MHE. DKT. ANGELINE S. L. MABULA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga uzio katika Shule za msingi ambazo hazina uzio maeneo ya mijini?
Supplementary Question 1
MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, kwa kuwa Serikali imefanya kazi nzuri sana kutoa hela hizo, lakini je, Jimbo la Ilemela limefanikiwa katika fungu hilo?
Swali la pili, kwa kuwa shule nyingi za primary zipo barabarani, zikiwemo hata zile za vijijini na kule Kata ya Uru Kusini Shule ya Okaseni ipo barabarani kabisa, mpira ukiteleza tu gari linapita watoto wanapata ajali. Ni lini sasa itakuwa ni azimio muhimu kwamba shule zote za primary za mjini na vijijini zijengewe uzio? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, Jimbo la Ilemela ni moja ya majimbo ambayo yamenufaika kwa fedha ambazo zimepelekwa kwa ajili ya ujenzi wa uzio, zikiwemo hizi shilingi bilioni 5.57 ambazo Serikali imezitoa, lakini nitumie nafasi hii kuendelea kuwasisitiza wakurugenzi wa Mamlaka Serikali za Mitaa kwamba ni wajibu wao na wanawajibika kuhakikisha wanatambua shule zote ambazo zina mazingira hatarishi na kutenga fedha za mapato ya ndani kwa awamu kwa ajili ya kujenga uzio ili kuhakikisha watoto wetu wanakuwa salama zaidi na Serikali Kuu itaendelea kutoa fedha hizo kwa awamu ili kuhakikisha watoto wetu wanakuwa salama zaidi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, ni kweli zipo shule ambazo zipo kandokando ya barabara kuu na ni hatarishi zaidi kwa wanafunzi na Serikali ina mpango huo na imeanza kuutekeleza mpango wa kuzitambua shule ambazo zina mazingira hatarishi kwa maana ya geographical location, lakini pia kwa shule zile ambazo zina watoto wenye mahitaji maalumu na imeendelea kutenga bajeti kwa ajili ya ujenzi wa uzio.
Kwa hiyo, nikuhakikishie Mheshimiwa mama yangu, Mama Shally Raymond kwamba tutaendelea kufanya hivyo ili kuhakikisha watoto wetu wapo katika mazingira salama zaidi. (Makofi)
Name
Ng'wasi Damas Kamani
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SHALLY J. RAYMOND K.n.y. MHE. DKT. ANGELINE S. L. MABULA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga uzio katika Shule za msingi ambazo hazina uzio maeneo ya mijini?
Supplementary Question 2
MHE. NG'WASI D. KAMANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, imefanya mabadiliko makubwa ndani ya muda mfupi kuhakikisha inaendelea kumuinua mtoto wa kike katika elimu, ikiwemo kuwarudisha mabinti waliyokuwa wamepata ujauzito shuleni, lakini pia ujenzi wa shule 26 za wasichana katika mikoa yote ya Tanzania Bara. Sasa baadhi ya shule hizi bado hazina uzio, nini mkakati wa Serikali wa kuhakikisha shule hizi zinawekewa uzio ili kuendeleza ulinzi wa mtoto wa kike pale anapokuwa anapata elimu?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya mapinduzi makubwa katika sekta ya elimu kwa ujumla, lakini pia katika eneo la elimu ya mtoto wa kike kwa kujenga shule kubwa za sayansi za kila mkoa, shule 26 ambazo zote zimekamilika na watoto wetu wameanza kupata masomo katika maeneo hayo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge Ng'wasi Kamani, kwamba Serikali ilishaweka bajeti na ishaandaa master plan kwa ajili ya kujenga uzio kwenye shule zote za sekondari za mikoa ili kuhakikisha kwamba watoto wetu wanakuwa katika mazingira salama zaidi, lakini pia na shule nyingine ambazo zipo katika maeneo hatarishi.
Name
Priscus Jacob Tarimo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Moshi Mjini
Primary Question
MHE. SHALLY J. RAYMOND K.n.y. MHE. DKT. ANGELINE S. L. MABULA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga uzio katika Shule za msingi ambazo hazina uzio maeneo ya mijini?
Supplementary Question 3
MHE. PRISCUS J. TARIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana, kwa kuwa shule za sekondari na za msingi Moshi Mjini kupitia ma-group ya alumni pamoja na wananchi na wazazi wameanza kujenga ukuta na kwa kuwa na mimi pia nimeunga juhudi hizo kwa kuwapa shilingi milioni 4.5 shule nne; Shule ya Sekondari ya JK, Shule ya Sekondari ya Karanga, Shule ya Msingi Kiusa na Shule ya Sekondari Kiusa kila moja shilingi milioni 4.5 kuunga mkono juhudi hizo. Je, Serikali ipo tayari sasa kuwasaidia wakamilishe kuweka uzio katika shule hizo? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, kwanza, nimpongeze sana Mbunge wa Moshi Mjini, Mheshimiwa Tarimo kwa kutoa kiasi hicho cha shilingi milioni 4.5 kuunga mkono juhudi za wananchi, wazazi na alumni ambao wanachangia kwa ajili ya ujenzi wa uzio katika shule hizo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nikuhakikishie tu pamoja na jitihada hizo za wananchi, Mbunge pamoja na wadau Serikali pia imeendelea kupeleka fedha kwa ajili ya ujenzi wa uzio katika maeneo hayo na nikuhakikishie Mheshimiwa Mbunge na Wananchi wa Jimbo la Moshi Mjini kwamba Serikali itaendelea kutenga fedha kwa awamu ili kuunga mkono juhudi hizo na kuhakikisha kwamba shule hizo zinajengewa uzio. (Makofi)
Name
Husna Juma Sekiboko
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SHALLY J. RAYMOND K.n.y. MHE. DKT. ANGELINE S. L. MABULA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga uzio katika Shule za msingi ambazo hazina uzio maeneo ya mijini?
Supplementary Question 4
MHE. HUSNA J. SEKIBOKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana, pamoja na tatizo hilo la uzio katika shule za mijini, zipo shule za vijijini pia ambazo zinakosa uzio na zipo hatarini kuingiliwa na wanyama wakali pamoja na mifugo kama ng’ombe. Je, ni upi mkakati wa Serikali kuhakikisha kwamba shule za vijiji na zenyewe zinawekewa uzio? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kimsingi Serikali iliweka mpango wa kujenga uzio katika shule zetu zote kwa awamu, lakini kwa kipaumbele ni zile shule zenye mazingira hatarishi zaidi bila kujali ni shule za mijini au vijijini ilimradi mazingira yake ni hatarishi zaidi basi Serikali imeendelea kuweka kipaumbele zaidi kwa ajili ya ujenzi wa uzio.
Kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba hata shule za vijijini ambazo zina mazingira hatarishi zaidi zimepewa kipaumbele na zipo shule ambazo tayari zimejengewa uzio na zoezi hili ni endelevu Serikali itaendelea kuteka fedha kwa ajili ya kujenga uzio katika shule hizo ili kuhakikisha usalama kwa wanafunzi. (Makofi)