Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 21 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 266 2025-05-09

Name

Bupe Nelson Mwakang'ata

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question


MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA Aliuliza: -

Je, lini Mradi wa Umwagiliaji Bonde la Rukwa wenye thamani ya shilingi bilioni 21 utakamilika?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, ujenzi wa Skimu ya Ilemba wenye thamani ya shilingi bilioni 21 ulitarajiwa kukamilika mwezi Disemba, 2024. Hata hivyo, ujenzi huo haukukamilika kutokana na mvua za El-Nino za mwaka 2023/2024 pamoja na mvua nyingi za masika zinazoendelea mkoani Rukwa kwa sasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imefanya tathmini ya muda uliopotea kutokana na mvua nyingi zilizosababisha kusimama kwa kazi na kuongeza muda wa utekelezaji wa mradi hadi mwezi Disemba, 2025. Ili kuhakikisha mradi unakamilika kwa muda uliopangwa, Tume itaendelea kumsimamia mkandarasi husika kwa karibu. (Makofi)