Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Bupe Nelson Mwakang'ata

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA Aliuliza: - Je, lini Mradi wa Umwagiliaji Bonde la Rukwa wenye thamani ya shilingi bilioni 21 utakamilika?

Supplementary Question 1

MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza haya maswali mawili ya nyongeza. Kwanza, kabisa niipongeze sana Serikali kwa kututengea fedha nyingi sana shilingi bilioni 21 siyo kitu kidogo, tunawashukuru sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilitaka kujua sasa Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha kwamba mradi huu unakamilika kwa wakati, kwa sababu wananchi walikuwa wana mategemeo makubwa sana kutokana na ukame uliojitokeza. Kwa hiyo, walikuwa na mategemeo makubwa sana na mradi huu. Ni lini sasa Serikali itahakikisha mradi huu unakamilika?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, Wilaya ya Nkasi, Jimbo la Nkasi Kusini halijapata mradi wa umwagiliaji hata mmoja. Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha na jimbo hilo linapata mradi mmoja wa umwagiliaji? Ahsante. (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer


NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na mimi nimpongeze sana dada yangu Mheshimiwa Bupe Mwakang’ata kwa kazi nzuri ya kufuatilia miradi katika Mkoa wake wa Rukwa hususani ya kilimo. Jambo moja tu nimthibitishie kwamba huu mradi utakamilika kama tulivyopanga inapofika Disemba mwaka huu, kwa sababu fedha tumeshampatia mkandarasi na tumeshawaelekeza watu wa Tume katika Kanda ile ya mkoa wenu kuhakikisha wanafuatilia kwa karibu ili wale wananchi wa kule bondeni waweze kufaidika na huu mradi. Kwa hiyo, tutaendelea kufuatilia kwa karibu kuhakikisha unakamilika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kulipatia mradi Jimbo la Nkasi Kusini kwa ndugu yangu Mheshimiwa Mbogo, nikushukuru sana Mheshimiwa Mbunge wa Viti Maalum kwamba hili jambo lipo na tunafanya tathmini katika yale maeneo ambayo yanafaa. Tukishamaliza ile tathmini maana yake tutajenga miradi kama ambavyo wewe umetoa maelezo na Mbunge alishatuletea maombi katika eneo hilo, ahsante sana. (Makofi)

Name

Abdallah Dadi Chikota

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nanyamba

Primary Question

MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA Aliuliza: - Je, lini Mradi wa Umwagiliaji Bonde la Rukwa wenye thamani ya shilingi bilioni 21 utakamilika?

Supplementary Question 2

MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru, kwa kuwa mkandarasi atakayejenga Mradi wa Arusha Chini uliopo Kata ya Chawi na Kiromba ameshapatikana. Je, ni lini utekelezaji wa mradi huu utaanza? (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, ni kwamba ninatambua mradi huu kwenye Jimbo la Mheshimiwa Chikota, upo katika hatua ya mkandarasi kufanya mobilization kupeleka vifaa kwa sababu tayari tumeshamlipa advance payment. Kwa hiyo, nimthibitishie tu kwamba tutamharakisha mkandarasi ili anze kazi, ahsante. (Makofi)

Name

Dr. Charles Stephen Kimei

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Vunjo

Primary Question

MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA Aliuliza: - Je, lini Mradi wa Umwagiliaji Bonde la Rukwa wenye thamani ya shilingi bilioni 21 utakamilika?

Supplementary Question 3

MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, nimpongeze sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa kutembelea Jimbo la Vunjo na kujionea kero nyingi kwenye masoko yetu, lakini pia kuona lile Bwawa la Urenga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimuulize Mheshimiwa Naibu Waziri kama bwawa hili ambalo lina uwezo mkubwa wa kuwezesha kilimo cha uwangiliaji kwenye Kata ya Kirua Vunjo Mashariki kama hili bwawa limeingizwa sasa kwenye bajeti ya mwaka huu? (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, ni kwamba ni kweli nilipita Vunjo kwa Mheshimiwa Dkt. Kimei na tulitembelea hilo Bwawa la Kweka na tuliona kabisa umuhimu na tuliwaelekeza watu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji katika mkoa wake kufanya tathmini na wameshafanya tathmini wameshatuletea. Tunachofanya sasa hivi ni kutafuta fedha ili tathmini hiyo ifanyike ili sasa tuweze kwenda kuliongeza upana na wale wananchi waweze kufaidika na mradi ule wa eneo la Kirua Vunjo, ahsante. (Makofi)

Name

Selemani Moshi Kakoso

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpanda Vijijini

Primary Question

MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA Aliuliza: - Je, lini Mradi wa Umwagiliaji Bonde la Rukwa wenye thamani ya shilingi bilioni 21 utakamilika?

Supplementary Question 4

MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, Scheme ya Karema ni ya muda mrefu na Serikali iliahidi kutoa fedha kwa ajili ya kuikamilisha hiyo scheme, ni lini Serikali itapeleka fedha walizoahidi shilingi bilioni 30 kwa ajili ya kukamilisha scheme hiyo? (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, ni kweli tunatambua umuhimu wa Scheme ya Karema na hatua ambayo tunamalizia ni kufanya tathmini ili sasa tupeleke fedha kwa sababu scheme ile ni kubwa sana na itakuwa na faida kubwa kwa wananchi wa jimbo lake. Kwa hiyo, nimwondoe tu shaka Mheshimiwa Mbunge kwamba hili tunalitambua na tumelipa umuhimu mkubwa. (Makofi)

Name

Mohamed Lujuo Monni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chemba

Primary Question

MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA Aliuliza: - Je, lini Mradi wa Umwagiliaji Bonde la Rukwa wenye thamani ya shilingi bilioni 21 utakamilika?

Supplementary Question 5

MHE. MOHAMED L. MONNI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, mwaka 2024/2025 tulipitisha bajeti hapa na zikatengwa fedha kwa ajili ya Bwawa la Ndoroboni na Babayo katika Halmashauri ya Wilaya ya Chemba, ninaomba kujua ninaona bajeti inaishia kikomo mwezi wa sita na mpaka leo ujenzi haujaanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujua ni lini watatoa fedha ili kuanza ujenzi wa mabwawa hayo?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, ni kweli anachokisema Mbunge wa Jimbo la Chemba Mheshimiwa Monni. Haya mabwawa tulishayaweka katika bajeti yetu na kiukweli tulishatangaza kupata kwa ajili ya ukandarasi na tumeshaomba fedha Wizara ya Fedha na wametuahidi kutupatia na kwa sababu mwaka wa fedha bado mpaka mwisho wa mwezi wa sita, tutapeleka fedha ili miradi hii ianze kutekelezwa. (Makofi)

Name

Benaya Liuka Kapinga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbinga Vijijini

Primary Question

MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA Aliuliza: - Je, lini Mradi wa Umwagiliaji Bonde la Rukwa wenye thamani ya shilingi bilioni 21 utakamilika?

Supplementary Question 6


MHE. BENAYA L. KAPINGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, Mradi wa Umwagiliaji Kata ya Litumbandiosi kwa muda mrefu upo kwenye upembuzi yakinifu, ni lini sasa utaanza kujengwa?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, nimthibitishie tu Mbunge wa Jimbo la Mbinga Vijijini, Mheshimiwa Benaya kwamba mradi huu sisi tumeshamaliza tathmini ya mwisho na sasa hivi tupo katika hatua ya kumtafuta mkandarasi kwa ajili ya kuanza ujenzi. Kwa hiyo, wathibitishie tu wananchi wako kwamba mradi ule utajengwa na jitihada zile kubwa na wewe ni sehemu ya watu ambao wameifanya, ahsante. (Makofi)