Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 21 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 267 2025-05-09

Name

Salim Mussa Omar

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Gando

Primary Question

MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI K.n.y. MHE. SALIM MUSSA OMAR Aliuliza: -

Je, ni upi mpango wa Serikali kuifanya NFRA kujitegemea hususan Idara ya Vyakula ili kuepuka uhaba wa chakula pindi nchi tegemezi zinapokumbwa na majanga?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO Alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuimarisha uwezo wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ili ijitegemee na kupunguza utegemezi wa Serikali bila kuathiri jukumu lake la msingi la kuhakikisha usalama wa chakula nchini, Serikali ina mikakati ifuatayo:-

(i) Kuongeza uwezo wa kuhifadhi chakula kutoka tani 776,000 wa sasa hadi tani 3,000,000 ifikapo mwaka 2030. Hatua hiyo itafikiwa kwa kukarabati na kujenga vihenge na maghala ya kisasa na hivyo kuwezesha kudhibiti upotevu wa mazao baada ya mavuno;

(ii) Kuimarisha mifumo ya ununuzi na usambazaji ikiwemo matumizi ya TEHAMA ili kuongeza ufanisi na kuhakikisha upatikanaji wa chakula kwa haraka katika maeneo yenye changamoto; na

(iii) Kuimarisha uwezo wa kibajeti kwa kuongeza vyanzo vya mapato ikiwemo uzinduzi wa Hati Fungani ya Usalama wa Chakula (Food Security Bond). Hati hii inalenga kuongeza mtaji kwa ajili ya uboreshaji zaidi wa miundombinu, upanuzi wa shughuli za kibiashara na utekelezaji wa mikakati ya muda mrefu ya usalama wa chakula nchini.