Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 21 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 268 2025-05-09

Name

Joseph Zacharius Kamonga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ludewa

Primary Question

MHE. JOSEPH Z. KAMONGA Aliuliza: -

Je, lini ujenzi wa barabara ya Mkiu – Liganga – Madaba utaanza kwa kiwango cha lami kwa kuwa uwekezaji wa Liganga upo mbioni kuanza?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI Alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa Barabara ya Mkiu – Liganga – Madaba yenye urefu wa kilometa 112 imekamilika. Kwa sasa Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuijenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami.