Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Joseph Zacharius Kamonga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ludewa
Primary Question
MHE. JOSEPH Z. KAMONGA Aliuliza: - Je, lini ujenzi wa barabara ya Mkiu – Liganga – Madaba utaanza kwa kiwango cha lami kwa kuwa uwekezaji wa Liganga upo mbioni kuanza?
Supplementary Question 1
MHE. JOSEPH Z. KAMONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru sana kwa majibu ya Serikali na ningependa kuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa Serikali bado inatafuta fedha kwa ajili ya hii Barabara ya Mkiu – Liganga – Madaba na ile inayopita Liganga inayouganisha Mchuchuma kupitia Ibumi, je, Serikali haioni haja ya kuongeza fedha kwa ajili ya matengenezo ya kawaida hasa maeneo yale ya Ligangalanzuki pale Shaurimoyo na kule Ndolela upande wa Madaba ili shughuli za wananchi zisiathirike?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, barabara ile ya Itoni – Ludewa – Manda, sehemu ya Itoni - Lusitu imesimama kwa muda mrefu, mimi na Mheshimiwa Mwanyika tumekuwa tukiisemea sana na sasa Chama cha Wasafirishaji Abiria Mkoa wa Njombe wameandika barua kwamba wana kusudio la kusitisha usafiri wa wananchi maeneo yale. Je, ni lini barabara hii itaweza kuendelea kutengenezwa na je, Serikali ipo tayari kukutana na hawa Chama cha Wasafirishaji Abiria Mkoa wa Njombe? (Makofi)
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsnate, ninaomba kujibu maswlai mawili ya Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba hii barabara aliyosema ni moja ya barabara ya kimkakati kwa maana ya nchi kwa sababu ndiyo inayoenda ambapo kuna uwekezaji mkubwa sana wa chuma na wakati Serikali inatafuta chanzo cha uhakika cha fedha ili tuweze kuijenga hii barabara ambayo sehemu hii tunajenga kwa utaratibu wa zege kwa sababu ya ukubwa wa mzigo utakaotoka huko, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tumetenga fedha za kuhakikisha kwamba barabara hii inapitika na tambua kwamba sasa hivi mvua zinanyesha nyingi sana, lakini tulishawaelekeza mameneja, na labda nitumie nafasi hii kuhakikisha kwamba fedha zilizotengwa katika kipindi hiki hasa cha mvua wanaendelea kufanya matengenezo ili kufanya barabara hizi zipitike japo katika kipindi hiki cha mvua huwa hatuwekezi fedha nyingi sana kwa sababu hasa kwenye hizi barabara ambazo sio za lami kwa sababu unaweza ukawekeza halafu ikaondoka, tunafanya tu ili barabara hizi ziweze kupitika. Kwa hiyo, meneja alishaelekezwa afanye hivyo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala la Itoni - Lusitu, mkandarasi yupo site tumeshamlipa sehemu ya malipo ya fedha alizokuwa anadai na tuna uhakika kwamba muda sio mrefu tutakamilisha yale malipo yote ili aendelee kufanya kazi na tumeshampa maelekezo huyo meneja mahali ambako kuna diversion ahakikishe kwamba barabara hii inapitika muda wote, ahsante. (Makofi)
Name
Stanslaus Shing'oma Mabula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nyamagana
Primary Question
MHE. JOSEPH Z. KAMONGA Aliuliza: - Je, lini ujenzi wa barabara ya Mkiu – Liganga – Madaba utaanza kwa kiwango cha lami kwa kuwa uwekezaji wa Liganga upo mbioni kuanza?
Supplementary Question 2
MHE. STANSLAUS S. MABULA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, kwa kuwa usanifu wa Barabara ya Mwanza – Busisi ulishakamilika, tender ilishatangazwa na traffic ni kubwa sana, magari zaidi ya 15,000 kwa siku. Mheshimiwa Waziri ni lini Barabara ya Mwanza – Usagara mkandarasi atatangazwa na kuanza utekelezaji? (Makofi)
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, kwanza niwashukuru Waheshimiwa Wabunge kwa kupitisha bajeti na hata katika bajeti kujenga hii barabara kwa njia nne Mwanza ilitamkwa na ipo na ni mpango pia wa mwaka huu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, tulishampata mkandarasi ambacho tunafanya sasa hivi ni majadiliano (negotiation) ili tuweze kufikia kwenye maeneo ambayo tutakubaliana kwenye upande wa Serikali na yeye ili hatimaye sasa aanze kuijenga hiyo barabara. Kwa hiyo, ni kipaumbele kikubwa cha Serikali kupunguza msongamano katika Jiji la Mwanza ikiwa ni kuijenga hiyo barabara kwa njia nne, ahsante. (Makofi)
Name
Eric James Shigongo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Buchosa
Primary Question
MHE. JOSEPH Z. KAMONGA Aliuliza: - Je, lini ujenzi wa barabara ya Mkiu – Liganga – Madaba utaanza kwa kiwango cha lami kwa kuwa uwekezaji wa Liganga upo mbioni kuanza?
Supplementary Question 3
MHE. ERICK J. SHIGONGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa kuniona.
Kwa kuwa Mheshimiwa Waziri alikuwepo tuliposaini mkataba na mkandarasi wa Barabara ya Sengerema – Nyehunge na kwa kuwa ilitokea changamoto kidogo kwenye mkataba ule Serikali ikaamua kutafuta mkandarasi mwingine, je, Mheshimiwa Waziri yupo tayari kuwaeleza wananchi wa Buchosa wamsikie mkandarasi amepatikana na kama amepatikana ataanza kazi lini?
MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu.
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, Mheshimiwa Mbunge alichosema ni kweli na tulishatangaza upya hiyo barabara na sasa tupo kwenye majadiliano na mkandarasi huyo mpya ili aweze kuanza kazi na tunategemea kabla ya tarehe 30 Juni tuwe tumeanza kazi hiyo ya kuanza kujenga hiyo Barabara ya Sengerema – Nyehunge. (Makofi)
Name
Halima James Mdee
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JOSEPH Z. KAMONGA Aliuliza: - Je, lini ujenzi wa barabara ya Mkiu – Liganga – Madaba utaanza kwa kiwango cha lami kwa kuwa uwekezaji wa Liganga upo mbioni kuanza?
Supplementary Question 4
MHE. HALIMA J. MDEE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni lini Barabara ya Mwai Kibaki inayounganisha Daraja la Mlalakuwa, linalounganisha Kawe Round About mpaka Africana itapanuliwa ili kupunguza foleni kwenye Jiji la Dar es Salaam?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, barabara alizozitaja zipo kwenye mpango wetu wa kuzijenga na itakuwa pia ni sehemu ya mipango yetu ya kupunguza msongamano wa Jiji la Dar es Salaam. Kwa hiyo, akiangalia hata kwenye vitabu vyetu hiyo barabara alizozitaja ni barabara ambazo zinaenda kutekelezwa. (Makofi)
Name
Aloyce John Kamamba
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Buyungu
Primary Question
MHE. JOSEPH Z. KAMONGA Aliuliza: - Je, lini ujenzi wa barabara ya Mkiu – Liganga – Madaba utaanza kwa kiwango cha lami kwa kuwa uwekezaji wa Liganga upo mbioni kuanza?
Supplementary Question 5
MHE. ALOYCE J. KAMAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Barabara ya Kakonko – Kinonko - Ruhuru – Nyakiobe – Guarama - Kabari mpaka wa Muhange, lini ujenzi wake utaanza kwa kiwango cha lami?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, barabara hiyo ni barabara muhimu ambayo pia inaunganisha na Mkoa wa Kagera, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, tukishakamilisha usanifu barabara hiyo tutaanza kuijenga kwa kiwango cha kami. (Makofi)
Name
Issaay Zacharia Paulo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbulu Mjini
Primary Question
MHE. JOSEPH Z. KAMONGA Aliuliza: - Je, lini ujenzi wa barabara ya Mkiu – Liganga – Madaba utaanza kwa kiwango cha lami kwa kuwa uwekezaji wa Liganga upo mbioni kuanza?
Supplementary Question 6
MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, ni miaka mitatu sasa kipande cha barabara ya Mbulu – Garababi kilometa 25 mkandarasi ameitelekeza na huduma ya usafiri imekuwa mbaya sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nini kauli ya Serikali kuhusu mkandarasi huyu ili kwenda kutengeneza hicho kipande kwa huduma ya kwanza ile ya barabara ya udongo na baadaye mradi wa lami? (Makofi)
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, barabara hii tayari ina mkandarasi na alishaanza kazi na nimhakikishie Mbunge na wananchi wa Mbulu tayari Serikali imeshamlipa sehemu ya malipo aliyokuwa anayadai. Kwa hiyo, nimwagize Meneja wa Mkoa wa Mara kuhakikisha kwamba anamwimiza mkandarasi arudi site na kuanza kuijenga na hasa yale maeneo yote yamekwama hasa zile diversion ili kusiwe na mkwamo wa usafiri katika eneo hilo. (Makofi)
Name
Amandus Julius Chinguile
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nachingwea
Primary Question
MHE. JOSEPH Z. KAMONGA Aliuliza: - Je, lini ujenzi wa barabara ya Mkiu – Liganga – Madaba utaanza kwa kiwango cha lami kwa kuwa uwekezaji wa Liganga upo mbioni kuanza?
Supplementary Question 7
MHE. AMANDUS J. CHINGUILE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushuru na tunaishukuru Serikali kwa kuipandisha hadhi kipande cha barabara kutoka Kilimarondo kwenye Lumesule, ni nini mpango wa Serikali kujenga barabara ya kutoka Kilimarondo – Bondo – Nachingwea kwa kiwango cha lami?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ikishapandishwa hadhi kwanza ni kuijenga na kuiweka katika barabara ambazo zina hadhi ya TANROADS na baada ya hapo barabara hiyo itasanifiwa ikiwa ni mpango wa kuijenga kwa kiwango cha lami. Kwa hiyo, kwanza kutoka kwenye kiwango ilichokuwa cha TARURA lazima tuipandishe iwe kwenye viwango vya TANROADS, halafu tuisanifu kwa ajili ya kuijenga kwa kiwango cha lami, ahsante.