Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 21 Industries and Trade Wizara ya Viwanda na Biashara 270 2025-05-09

Name

Justin Lazaro Nyamoga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilolo

Primary Question

MHE. JUSTIN L. NYAMOGA Aliuliza: -

Je, lini Serikali itatimiza ahadi yake ya kujenga Kiwanda cha Chai cha Kilolo?

Name

Exaud Silaoneka Kigahe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kaskazini

Answer

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru, Serikali kwa kutambua umuhimu wa uwepo wa Kiwanda cha Chai Kilolo imefanikiwa kuvutia uwekezaji wa kiwanda hicho na uwekezaji umefanywa na Kampuni ya HongDingXin ya kutoka China. Kiwanda kina uwezo wa kuchakata tani 20 za chai kwa siku na kitatoa ajira 120 za moja kwa moja pamoja na kutoa soko la uhakika kwa wakulima wa chai katika Wilaya ya Kilolo na maeneo ya jirani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa ujenzi wa kiwanda hicho umekamilika na tayari wameshaanza majaribio tangu tarehe 28 Aprili, 2025, mara baada ya majaribio hayo kukamilika, tunaamini mpaka sasa watakuwa wameanza uzalishaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana.